Msaada wenu: Baba yangu mzazi anataka kunitimua kwenye nyumba ya babu yetu

Msaada wenu: Baba yangu mzazi anataka kunitimua kwenye nyumba ya babu yetu

Marehemu babu yangu kabla ya kufariki alisema kabisa na wazi kuwa nisinyanyasike kwenye ule mji.
Sasa si uende huko CCM wakupe nyumba, hiyo nyumba wewe haikuhusu. Nyumba ni yaya baba yako anayo haki ya kukutimua kwa huo umbavu wako.
 
Mhh aisee yaani unataka kujipendekeza CCM kwa kupitia nyumba ya Mzee ana haki kukutimua hakuna urithi kwa babu au bibi miaka 28 unafikiria Mambo ya nyumba ya baba aisee pambana ikiwezekana ondoka hapo utafunguliwa njia kuliko kukaa na kukariri ulithi wa babu utakufa masikini..nilipokua na umri wako nipo Lusaka napambana wala sifikirii viwanja wala nyumba za Wazee aisee...
 
Toka hiyo ndo tabia ya uchawi inavyoanza mtoto mdogo unawaza urithi na wanao waishi hapo hapo kachelewa isee
 
Kisheria nyumba ni ya baba ila kama kuna maandishi aliyoacha babu sawa. Tafuta tu chumba usibishane na baba.
 
Mzee wako ni mpinzani
Ila asikufanye ad ww ukose ad vocha kisa anaichukia CCM.
Vijana tunaangalia fursa siasa baadae
 
Duu yaani baba yako anaishi kwao na wewe unaishi kwa babu yako.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]umefikiria ka mm,alitazamia watu wamjaze upepo hapa akaweke ding ndan kisa cha nyumba ya babu yake

Tena ana bahati sisi bado tuna upendo
Mjadala huu ungekuwa kwenye social networks za nje angeuziwa na sumu au Pistol kabisa ammalize
Ashukuru sana kuna waungwana bado nyumbani [emoji56][emoji56]
 
Hapana mkuu hapo nyumbani kuna chumba ambacho mzee amekifunga na kufuli na kunitolea vitu nje, ananitukana eti bora apangishe hapate kodi kuliko mimi kukaa na kujaza choo
naona baba yako amepata mpangaji ambae hanyi hivyo choo hakita jaa
 
Duu yaani baba yako anaishi kwao na wewe unaishi kwa babu yako.
Babu amempa chumba na kumwambia asinyanyasike nae akapata kiburi,ni bora umwambie baba yako akupe nyumba yako ya urithi kisha wewe nawe umpangishe
 
Me naona mzee wako yuko sahihi kabisa,maana umemletea dharau sana..

Ningekuwa mimi aisee.
 
Maisha haya magumu. Unaanzaje kuchagua kazi? Hata kama unaichukua CCM siyo suala la kugombezana na mtoto kisa kujiingiza kwenye CCM. Watu siku hizi wanatafuta pesa na siyo chama. Popote pale kwenye pesa watu wataenda kufanya kazi. Huyo dingi hajatumia busara kabisa
Kwa hiyo ulitaka mdingi akenue meno kwa kufanywa msukule wa CCM?halafu uliwahi ona wapi ccm ikamjali mtu waliemtumia?
 
Habarini ndugu zangu wana JamiiForums, matumaini yangu mu wazima wa afya tele.

Nisiwachoshe niende kwenye mada moja kwa moja

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 28, nimemaliza chuo kikuu mwaka jana. Tangu nimemaliza chuo, nimehangaika sana kupata kazi bila mafanikio. Mwaka huu mwezi uliopita nilibahatika kupata kazi ya kuandikisha wapiga kura kwenye uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa.

Baba yangu alikataa kabisa nisijihusishe kwenye mambo yoyote yanayohusiana na siasa kwa hiyo hakupendezwa. Baada ya hilo zoezi la uandikishaji kuisha, juzi Ijumaa kuna mjumbe wa chama cha mapinduzi (CCM) aliniambia kuwa nimtafutie wanachama 20 tu kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, na kuahidi atanipa pesa ya maji.

Pale home jumla tupo watu 7 pamoja na ndugu wengine, nilitaka kwanza kuanza na familia yangu, nilimfuata baba yangu na kumueleza kuwa na yeye awe mmoja wapo katika watu 20 nilioombwa na mjumbe

Ndugu zangu, baba alinitukana matusi mazito, siwezi kuyaandika hapa, mpaka kufikia kuniambia nitakuwa nimelaaniwa na dunia. Kaenda mbali zaidi ananimbia kama ntashilikiana na watu wa CCM na kumhusisha yeye, ataniondoa kwenye nyumba tunayoishi, ukizingatia hiyo nyumba ni ya babu yangu ambaye yeye ni baba yake.

Marehemu babu yangu kabla ya kufariki alisema kabisa na wazi kuwa nisinyanyasike kwenye ule mji. Wakuu, mpaka ninapoandika hapa, baba atoa vitu vyangu nje, anasema nikahamie kwa huyo mjumbe.

Naombeni ushauri wenu wakuu, nataka kuipigania haki yangu, maana babu alisema kile chumba nilichokuwa nakaa ni mali yangu halali.

Nipo katika wakati mkuu, nisaidieni niende polisi au nifanye nini wakuu?

Asanteni.
Mkuu bora usepe
 
Kesi ya nyani umeileta kwa mkulima!

Acha nijiandae kusoma komenti watakutia hasira huku hadi ujikute unajuta kuandika uzi wako.
ungemwambia tu aende kwenye nyumba ya baba yake ili kuepusha shari
 
Tuanzie hapa: Anae acha urithi ni babu au baba..Babako kapewa urithi na baba ake, na wewe mwambie baba ako akupe urithi wako....na urithi si lazima kwaiyo akikunyima kuwa mpole
 
Back
Top Bottom