Msaada wenu: Baba yangu mzazi anataka kunitimua kwenye nyumba ya babu yetu

Msaada wenu: Baba yangu mzazi anataka kunitimua kwenye nyumba ya babu yetu

nenda lumumba kawaeleze matatizo yako watakusaidia
 
Ulishiriki vipi kuandikisha wakati Kanuni za Uchaguzi zinasema watakaoandikisha na kusimamia uchaguzi ni watumishi wa umma tu?
 
Wasomi wetu wa siku hizi ndio nyie?. Baba ana akili kukuzidi wewe?
 
Mrithi wa hiyo nyumba ni baba yako,si wewe.U msomi wa namna gani hata hili dogo tu linakushinda?
 
...Kyle kwetu Tanga tuliimba:

'Hayo maneno yenu,
Mmeyataka wenyewe,
Sasa mwaiona Ng'ondo (Vita)
Mwafunga milango...'!

Baba yako mzazi amekumbia Hataki ujihusishe na Mambo ya Siasa.
Haya, unajihusisha kinyemela...
Halafu bado unamfuata na kumuomba
Awe Mwanachama Wa Chama cha Siasa!!

...Ubaya mnautafuta wenyewe halafu wakichukua hatua, mnalalamika!!!
 
Mkuu we ni juha kabisa, anayrstshili kurithi hiyo nyumba ni baba yako na wala sio ww. Pia hapo ni nyumbani kwa baba yako ondoka ukatafute vyaku nyambafu we
 
Najua hukumaanisha. Mie pia nimeandika kuonesha Kuna aina mpya ya uandishi imezuka, tofauti na tuliyofundishwa darasani. Huya nasoma uchangiaji wako kwenye mijadala. Nafahamu sio uandishi wako huu
Jitahidi kuangalia hizi alama" "mie naandika for funny tu mkuu
 
Ufukuzwe tu hamna jinsi unaleta laana kwenye familia kwa kushirikiana na ccm
 
Mpumbavu kabisa wewe,yaani unampelekea Baba yako panya nyumbani wakati hawapendi na wewe unajua kabisa?anatakiwa akupe kipigo kikali sana Kwa kumdharau,unadanganyika na vicheji mbuzi shwain kabisa

[emoji23][emoji23]
 
Baada ya figisu za huu uchaguzi

Kila nikilala naota misisiemu yote imekufa, nikiamka naikuta

Nakasirika mnoo!
Kila nikiandika nafuta.

..........Hivi chama chetu kinajua kinachukiwa hivi mtaani?
 
Nenda tu kwa mjumbe umuombe akupe hata banda LA uani ujistiri,
Nyumba ni ya babu yangu, ananitisha eti akinikuta ndani atanimwagia maji ya moto, anasema nikaishi ukouko kwa mjumbe wa ccm
 
Mkuu umeona mbali,nimesoma comment za wadau nikakumbuka maneno yk
Kesi ya nyani umeileta kwa mkulima!

Acha nijiandae kusoma komenti watakutia hasira huku hadi ujikute unajuta kuandika uzi wako.
 
Habari hii inasikitisha kwa sababu nyingi sana.

1. Familia inafarakana.

2. Kijana wa miaka 28 anaishi nyumbani na baba yake.

3. Baba wa kijana mwenye miaka 28 naye anaishi nyumba ya baba yake.

4. Kijana wa miaka 28 anataka kula vichwa vya nyumbani ili apate faida.

5. Siasa zinafarakanisha familia.

6. Wahitimu wa vyuo hawana kazi za kueleweka.

7. Mafarakano ya kifamilia yanataka kupelekwa polisi.

8. Kijana wa miaka 28 anapangiwa kutoshiriki siasa, haki yake ya msingi ya kikatiba.

9. Vyama vya siasa vinatumia hela na ukosefu wa ajira kama mtaji wa kisiasa.

10. Umasikini mwanzo mpaka mwisho. Wa akili na mali.

[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji121]️Nime penda comment yako. I mejipambanua kama ana akili ameelewa
 
nyumba ya babu ni ya baba yako wewe katafute chako
[emoji15] Kama nyumba ya babu ni ya baba yake, Basi pasipo na Shaka ya baba yake ni ya kwake yeye[emoji847][emoji847]
 
Back
Top Bottom