Msaada wenu: Baba yangu mzazi anataka kunitimua kwenye nyumba ya babu yetu

Msaada wenu: Baba yangu mzazi anataka kunitimua kwenye nyumba ya babu yetu

Afadhali baba yako hiyo hela aliyokusomesa angenunua ng'ombe wengi afuge apate maziwa , kuliko kusomesha ling'ombe limoja ambalo halitoi hata maziwa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Umekuja kumshtak baba huku naenda kumuonesha ili akufukuze kabsa unatudhalilisha sisi wadogo zako hutak kumsikiliza baba
 
Habarini ndugu zangu wana JamiiForums, matumaini yangu mu wazima wa afya tele.

Nisiwachoshe niende kwenye mada moja kwa moja

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 28, nimemaliza chuo kikuu mwaka jana

Tangu nimemaliza chuo, nimeangaika sana kupata kazi bila mafanikio.

Mwaka huu mwezi uliopita nilibahatika kupata kazi ya kuandikisha wapiga kula kwenye uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa

Baba yangu alikataa kabisa nisijihusishe kwenye mambo yoyote yanayohusiana na siasa kwa hiyo hakupendezwa.

Baada ya hilo zoezi la uandikishaji kuisha, juzi Ijumaa kuna mjumbe wa chama cha mapinduzi (CCM) aliniambia kuwa nimtafutie wanachama 20 tu kwaajili ya maadalizi ya uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, na kuahidi atanipa pesa ya maji

Pale home jumla tupo watu 7 pamoja na ndugu wengine, nilitaka kwanza kuanza na familia yangu, nilimfata baba yangu na kumueleza kuwa na yeye awe mmoja wapo katika watu 20 nilioombwa na mjumbe

Ndugu zangu baba alinitukana matusi mazito, siwezi kuyaandika hapa, mpaka kufikia kuniambia nitakuwa nimelaaniwa na dunia.

Kaenda mbali zaidi ananimbia kama ntashilikiana na watu wa CCM na kumhusisha yeye, ataniondoa kwenye nyumba tunayoishi, ukizingatia hiyo nyumba ni ya babu yangu ambaye yeye ni baba yake

Marehemu babu yangu kabla ya kufariki alisema kabisa na wazi kuwa nisinyanyasike kwenye ule mji

Wakuu mpaka ninapoandika hapa, baba atoa vitu vyangu nje, anasema nikahamie kwa huyo mjumbe

Naombeni ushauri wenu wakuu, nataka kuipigania haki yangu, maana babu alisema kile chumba nilichokuwa nakaa ni mali yangu halali

Nipo katika wakati mkuu, nisaidieni niende polisi au nifanye nini wakuu?

Asanteni.
Kwa hio wewe unatumika na CCM sio?Nenda kalale Magogoni.
 
pole sana mkuu,,, nakushauri uende kwenye tawi lolote karibu na kwenu walipo makamanda wa green guard waje wamuresti dingi ako,
kazingua sana kudadadadadekiiii zake!
 
Habarini ndugu zangu wana JamiiForums, matumaini yangu mu wazima wa afya tele.

Nisiwachoshe niende kwenye mada moja kwa moja

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 28, nimemaliza chuo kikuu mwaka jana

Tangu nimemaliza chuo, nimeangaika sana kupata kazi bila mafanikio.

Mwaka huu mwezi uliopita nilibahatika kupata kazi ya kuandikisha wapiga kula kwenye uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa

Baba yangu alikataa kabisa nisijihusishe kwenye mambo yoyote yanayohusiana na siasa kwa hiyo hakupendezwa.

Baada ya hilo zoezi la uandikishaji kuisha, juzi Ijumaa kuna mjumbe wa chama cha mapinduzi (CCM) aliniambia kuwa nimtafutie wanachama 20 tu kwaajili ya maadalizi ya uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, na kuahidi atanipa pesa ya maji

Pale home jumla tupo watu 7 pamoja na ndugu wengine, nilitaka kwanza kuanza na familia yangu, nilimfata baba yangu na kumueleza kuwa na yeye awe mmoja wapo katika watu 20 nilioombwa na mjumbe

Ndugu zangu baba alinitukana matusi mazito, siwezi kuyaandika hapa, mpaka kufikia kuniambia nitakuwa nimelaaniwa na dunia.

Kaenda mbali zaidi ananimbia kama ntashilikiana na watu wa CCM na kumhusisha yeye, ataniondoa kwenye nyumba tunayoishi, ukizingatia hiyo nyumba ni ya babu yangu ambaye yeye ni baba yake

Marehemu babu yangu kabla ya kufariki alisema kabisa na wazi kuwa nisinyanyasike kwenye ule mji

Wakuu mpaka ninapoandika hapa, baba atoa vitu vyangu nje, anasema nikahamie kwa huyo mjumbe

Naombeni ushauri wenu wakuu, nataka kuipigania haki yangu, maana babu alisema kile chumba nilichokuwa nakaa ni mali yangu halali

Nipo katika wakati mkuu, nisaidieni niende polisi au nifanye nini wakuu?

Asanteni.
Habari hii inasikitisha kwa sababu nyingi sana.

1. Familia inafarakana.

2. Kijana wa miaka 28 anaishi nyumbani na baba yake.

3. Baba wa kijana mwenye miaka 28 naye anaishi nyumba ya baba yake.

4. Kijana wa miaka 28 anataka kula vichwa vya nyumbani ili apate faida.

5. Siasa zinafarakanisha familia.

6. Wahitimu wa vyuo hawana kazi za kueleweka.

7. Mafarakano ya kifamilia yanataka kupelekwa polisi.

8. Kijana wa miaka 28 anapangiwa kutoshiriki siasa, haki yake ya msingi ya kikatiba.

9. Vyama vya siasa vinatumia hela na ukosefu wa ajira kama mtaji wa kisiasa.

10. Umasikini mwanzo mpaka mwisho. Wa akili na mali.
 
Penye ugumu ndipo hapo hapo unatakiwa ukaze .Pambana utafute vyako mzee ajafa unataka kumrithi
 
Kaka achana na siasa kama inakuharibia udugu. Kwanza ccm inakutumia kwa muda huu uchaguzi ukiisha utatupwkama dekio baada ya kupiga deki.
 
Kwa kweli kwa kijana mdogo kama wewe mwenye umri wa miaka 28 tu mi naona baba anakosea kukuambia uhame hapo nyumbani. Yeye anategemea kwa umri wako huo mdogo we utaenda wapi na ndio kwanza umemaliza chuo kikuu mwaka jana? Baba alitakiwa akuache kwenye kile chumba ambacho babu alikuachia na akasema usinyanyasike hapo nyumbani. Mimi nakushauri ukamripoti baba kwa mjumbe wa nyumba 10 ili uruhusiwe kuendelea kukaa hapo angalau kwa miaka 15 ijayo ili uwe umeshajipanga.
Miaka 28 ni mdogo [emoji3][emoji3][emoji3][emoji23]
 
Una miaka 28 na umemaliza chuo kikuu na umekosa kazi alafu unataka kumletea ccm baba yako nyumbani!! Really? Babako anajua kua sababu ya msingi ya wewe kukosa kazi ni ccm. Nyambafu wewe.
 
Maisha haya magumu. Unaanzaje kuchagua kazi? Hata kama unaichukua CCM siyo suala la kugombezana na mtoto kisa kujiingiza kwenye CCM. Watu siku hizi wanatafuta pesa na siyo chama. Popote pale kwenye pesa watu wataenda kufanya kazi. Huyo dingi hajatumia busara kabisa
Niko upande wa baba ako, hivi kweli hufikirii chanzo cha wewe kukosa ajira ni c.c.m? Watu wanapotea, wanakufa na wanatumbuliwa hovyo kila siku huoni? Ungekaa na baba ako vizuri akakueleza sababu kuliko kujimwambafai na degree yako
 
Huyo Mzee wako kakuchoka tu likely utakuwa kula kulala hayo mambo ya siasa kaona ndo nitoke vipi!

Toka kapigane wapo wengi tu walioletewa hila na wazee wao na leo wana maisha yao.

Kikubwa ukitusua halafu akaja kujilizaliza mfungie vioo liwe fundisho kwa wazee wengine wasiojielewa.

Mtu upo uzeeni halafu una-entertain mifarakano kwa watakaokulea muda si mrefu.
 
Back
Top Bottom