@kikoozi,aisee doctor nimepigika xana,hebu niazime elfu 50 ntakurejeshea salary ikitoka pls
Sorry naomba uniazime 50 then ntakurefund.. Nna shida plz.
Me nimekwama,niazme hamsin basi niweke Jambo langu Fulani sawa natkurudishia tarehe ishirini na tatu inshallah.
Hizo ni sms za ndugu 3 tofauti waliniomba niwakopeshe mwaka jana wakidai watanilipa ila hadi sasa hawajanilipa hata mmoja na mimi siwadai.
Kuna watu(wazazi, ndugu n.k) huwa hawakopeshwi, ila wanapewa. Akikurudishia ni sawa, asipokurudishia ni sawa pia.
Kwa yule atakayekurudishia, maamuzi ya kupokea yatakuwa juu yako, ama umwambie hiyo hela baki nayo au kama na wewe hali sio nzuri basi utaipokea ili usolve mambo yako.
Kama kipato chako kipo vizuri haina haja ya kuwakomalia ndugu kuwadai hela uliyowapa, toa tu kuwasaidia.
Kuna baadhi ya ndugu wanakuwa na tabia ya kuwakopa wenzio hela wakidai watawarudishia ila hawarudishi jambo ambalo linakuwa ni kero kwani anakuwa na tabia ya kuomba/kukopa mara kwa mara.
Mimi nikikopa(huwa naanza kukopa kwa watu wa karibu(ndugu)) huwa nawarudishia kulingana na jinsi nitakavyoahidi. Hadi hapo moyo wangu utakuwa na amani kwani sipendi kudaiwa mara kwa mara, ni kero sana.
Mkuu usihangaike kumdai mzee hiyo hela ila muombe tu hela akuwezeshe ili ukaanze life lako, hapo hawezi kukataa kukupa na akikupa hata kidogo wewe unaweza kuihesabu kama kakulipa lile deni ulilokuwa unamdai