Msaada wenu Wataalam au kama aliwahi kutibiwa na ukapona, ushauri wako utasaidia

Msaada wenu Wataalam au kama aliwahi kutibiwa na ukapona, ushauri wako utasaidia

Alipima akakutwa na H pylori na kuhusu Ant acid anatumia na akinywa maumivu upungua
Sasa kumbe na amepima kabisa. Alipewa dawa gani ? Maana shida ni vidonda vya tumbo, ishu ipo kwenye dawa, sidhani kama alimaliza dozi au anatumia dawa sahihi.
 
Wasalaamu ndugu. Poleni na mihangaiko ya kila mara. Binafsi siumwi, ila rafiki yangu anaumwa sana kama nitakavyoelezea hapa chini.

NOTE; Pamoja na kuumwa kwake huku kama hajakwambia huwezi jua kama anaumwa, sababu anatembea ni mzima kama wewe msomaji ulivyo hapo ukimuangalia kwa macho. Ila nimeshirikiana Naye kwenda kwa Madaktari, Hospitali mbalimbali kufanya vipimo vingi matokea yanatoka tofauti, na kama ikionekana labda anasumbuliwa na ugonjwa uliogundulika akipewa dozi bado hali inabaki kuwa ileile.

*MATATIZO YANAYOMSUMBUA* *( DALILI )*

Mwili kuchoka, kuuma (ususani upande wa kifua & mgongo ). Maumivu makali katikati ya tumbo na kifua na wakati mwingine baadhi ya sehemu za mwili upata ganzi mfano akikaa miguu ufa ganzi, mdomo kuchacha na kusikia vichomi,.

Tunaomba msaada wenu. Mungu awabariki

Bado hamjapata ufumbuzi
Kama bado tafadhali nicheki nikusaidie
 
Mbona hizo ni dalili za ulcers live mnahangaika na nini sasa? Aacha vyakula vinavyoongeza acidity na apate ushauri zaidi hospital.. acha ku google dawa nenda hospital mzee
 
Niko tofauti kidogo, Jamaa yako alikuwa mtu wa mazoezi sana? Naomba jibu.
Mimi pia nasumbuliwa na hizo dalili ikiwemo kupepesuka nikitembea..

Kama ulivosema ulivo uliza Mimi nilikua mtu wa mazoezi sana Sanaa nilikua nafanya mazoezi mpaka watu wakasema nazidisha Ila baadae niliacha Kama miezi mi tatu hivi
 
Back
Top Bottom