Msaada: Zawadi kwa atakayeweza kuwatambua watu hawa pichani

Msaada: Zawadi kwa atakayeweza kuwatambua watu hawa pichani

Bahari beach kuna uzi mwingine nimeweka video labda mods watanisaidia kuunganisha...ni kundi la vijana takriban nane wana silaha za jadi pia za moto wanavamia nyumba asubuhi na mchana
🤔🤔🤔...
 
Mimi kila siku nasema, utaalamu wa ufungaji wa kamera unasumbua wengi namna ya kuseti "macho".

Jambo la pili ni kutopata ushauri wa kitaalamu eneo lako hilo unalotega linatakiwa kuwekwa "macho" mangapi ili kupata picha zinazosomeka kwa urahisi nk nk.

Kwa picha hii labda wanaoweza kukusaidia ni majirani zako mbali mbali wa eneo unaloishi, tena kwa kuwawekea video.
 
Ungeweka na hiyo video pia.
Ila CCTV imefeli hapo kwenye kufunika sura za waalifu. Yaani kofia inapunguza uwezo wa CCTV kwa kiasi kikubwa kumpata mwizi kwa haraka.
Pengine shida budget.

Zingefungwa kila angle asingechomoa.
 
Pamoja na kwamba Picha za cctv hazionyeshi vizuri na kwamba wamejifunika na kofta ila kama unawafahamu utawafahamu tu zawadi nono itatolewa asanteniView attachment 2078242

cctv ni kazi bure kujua sura bali kuona tukio tu.labda nenda polisi maeneo ya karibu na kwako watajua huyu mwizi ni wa aina gani.sasa mtu yupo kigoma aje kutambua mtu wa dar tena mzaramo
 
Njia sahihi ya kudeal na muhalifu wako ni kumuendea kwa mganga tu
Hizi nyingine sijui cctv ni ngumu sana hata mahakamani huwezi thibitisha kirahisi[emoji23][emoji23]
 
Ushahidi wa kutumia CCTV hata kule mahakamani kwenye kesi ya Sabaya unasumbua watu.

Hapo kama mtu anamfahamu huyo muhalifu atamtambua licha ya hiyo kofia aliyovaa, na sura yake kwa mbali inaonekana, tatizo ni pale utakapotakiwa kuthibitisha bila kuacha shaka, ndio kazi itapoanzia.
Electronic evidence act
 
Swali langu ni kwamba

1.Ndani ya hiyo nyumba hakukuwa na kamera nyingine iliyowanasa vizuri?,maana naona ni kamera ya nje tu.

2.Jaribu kueleza ni nini kimetokea,unaposema arm robbery pasipo kueleza kiundani unatuacha na maswali!.

3.Nadhani kuleta huu uzi hapa ni kuhitaji msaada,sasa wewe unafichaficha habari unataka msaada upi?


Kwa kifupi ni kwamba hao watu mnafahamiana nao na ndiyo maana hutaki kueleza ukweli unaficha ficha,hiyo kamera inaonyesha kabisa wanakufahamu na hapo kama ni kwako wamekuja wakiwa na ramani kamili.
Wana Silaha za moto na za jadi ni kundi la takriban watu nane wamechukua gari ikiangalia post yangu ya nyuma utaona maelezo mengi yataharibu kama ykiwafahamu msaada wako utatosha
 
Jamani tunashukuru sana kwa ushiriakiano wenu kumtambua mharifu wetu. Wengi wamezunguzia mahakamani. Nataka niwatoe wasiwasi,sisi hatutaki kwenda mahakamani. Wewe ukituthibitishia tu ni huyu,basi kazi imeisha. Mengine atayamaliza mwenyewe tukimtia mkononi. Kwanza kutoka hapa kwetu mpaka mahakamani ni mbali.
 
Back
Top Bottom