Msafara wa Mwenge kusimamisha safari za mabasi Kwa masaa 4 ni udikiteta.

Msafara wa Mwenge kusimamisha safari za mabasi Kwa masaa 4 ni udikiteta.

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Nimetoka kijiji cha Kirando wilaya ya Nkasi alifajiri saa 12 Kwa basi la Rukwa Raha. Tumefika kijiji cha Chala majira ya saa 2 hivi asubuhi. Cha kushangaza tumekuta mabasi yamesimamishwa hapa Tangu saa 1 asubuhi Kwa Kisingizio cha kutoingilia msafara wa Mwenge àmbao unatokae Sumbawanga. Kutoka hapa Hadi yalipokuwa yanafanyika makabidhiano ya Mwenge ni kM 45-50.
Mpaka ninavyoandika mabasi yanayotoka Mpanda kwenda Mbeya nayo yako hapa yakisubiri Mwenge upite hapa saa 6 mchana. Hivi huu ukoloni wa kupotezeana Muda na kuharibu ratiba za wengine Polisi mmeamua kuwa wababe Kila mahali? Unawezaje kusimamisha magari ya abiria msafara uko km50 toka eneo lingine? Mnataka tuseme mtutafutie sababu??
Nakumbuka Makamu wa Rais Aliwahi kuzuia ukiritimba huu na ukasitishwa Kwa Muda. Lakini baada ya serikali kubaliki ubabe wa Polisi Sasa wamerejesha ukiritimba unaoweza hata kupoteza maisha ya wagonjwa wanaosafiri kufuata rufaa hospitali ya mkoa Sumbawanga.
 
Mimi binafsi sioni faida ya mwenge,
Hizo kazi zingeweza kufanywa na wakuu wa wilaya kuokoa gharama na usumbufu kwa wananchi
 
Back
Top Bottom