Msafara wa Raisi (Presidential Motorcade) kukosea njia! Hii imekaaje kiusalama?

Msafara wa Raisi (Presidential Motorcade) kukosea njia! Hii imekaaje kiusalama?

Heko wadau wa ulingo huu usio na mashabiki wengi.

Siku tatu zilizopita nilienda Mwanza kikazi, ndipo leo muda wa saa 4 au saa 5 asubuhi, tarehe 4 mwezi wa 9, 2018 nimeshuhudia kwa macho yangu msafara wa Raisi wa Tanzania ukikosea njia pale Mwanza kwenye Roundabout iliyoko karibu na BOT MWANZA.
View attachment 856842

Pamoja na kuwa walikuwepo askari wa usalama barabarani lakini nimeshangazwa kuona gari za mbele kusimama ghafla baada ya kuwa zimeingia junction ya Musoma road badala ya kunyooka na Airport road. Baada ya kusimama ghafla gari ya mbele ilipiga honi karibia mara nne, ambapo nafikiri ilimaanisha kutaka msaada wa kuelekezwa njia baada ya kukosea njia sahihi.

Ndipo mmoja wa askari kwenye gari la pili akashuka haraka na kumuonyeshea ishara ya kugeuza ili waendelee na Airport road. Wakati hayo yakiendelea ilibidi msafara wa gari za mbele usimame huku gari za nyuma zikipunguza mwendo kwa ghafla.

Baada ya kushuhudia tukio hilo nikabaki najiuliza maswali mengi, hivi kumbe somo la mawasiliano ni shida hata kwa taasisi nyeti ambazo zinaongoza msafara wa Raisi?


Je mawasiliano ya askari wa usalama barabarani yalikuwa hacked na kupoteza umakini wa taarifa na maelekezo?

Lakini pia nikajiuliza hili tukio kiusalama lina madhara gani?

Karibuni wadau.
Rais alishapotea njia kuongoza nchi siku nyingi.

Hao madereva wanamfuatisha tu style yake.
 
Kwani wewe uko kwenye right track?

Anyway huo ni uzembe wa hali ya juu kwa sababu kila mahali anapoenda kiongozi mkuu waliopo hapo(wenyeji) ndio huwa wanakuwa mbele (police) wakijua wanakokwenda.

Sasa hapo sijui mkuu ndio aliona mahindi ya kuchoma au matikiti akaamua kuwasimamisha mimi sijui maana hata clip imegoma kufinguka kwa na assume tu
 
Siku ikatokea rais akashambuliwa nchini wakuu wa polisi eneo husika na mashushushu wanaofanya kazi eneo husika inatakiwa wapandishwe kizimbani
 
Back
Top Bottom