Msafara wa Raisi (Presidential Motorcade) kukosea njia! Hii imekaaje kiusalama?

Msafara wa Raisi (Presidential Motorcade) kukosea njia! Hii imekaaje kiusalama?

Ngoja nikuache maana asili ya Mtanzania ni maneno mengi ,huku hamna kitu
Hivi...hujiulizi kwa nini inasemekana binadamu wa kwanza aliishi Tanzania? Sisi watanzania tunauwezo sana tu..! sema kutokana na hila za wasiotutakia mema ndizo zimetufikisha hapa. Yaani wewe kama ni mtanzania usijidharau hata kidogo. Wewe una uwezo mkubwa sana wa kufikiri na kutatua matatizo yanayokukabili, jishughulishe tu utaona matokeo yake.
Jioni njema.
 
Mbona hata wewe mleta mada umekosea majina ya barabara hizo?
 
Nakumbuka ilikua ni ziara mkoani Mara( Tarime kama sikosei) mwanamama akaupoteza msafara wa rais. Kwa mujibu wa taarifa alikamatwa akawekwa ndani ila kesho yake vyombo vya habari viliripoti kuwa amejiua kwa kujipiga risasi. Walisema alichukua bunduki counter akaji tyu tyu..
Alafu akaanguka Pyu pyu..
 
Hivi...hujiulizi kwa nini inasemekana binadamu wa kwanza aliishi Tanzania? Sisi watanzania tunauwezo sana tu..! sema kutokana na hila za wasiotutakia mema ndizo zimetufikisha hapa. Yaani wewe kama ni mtanzania usijidharau hata kidogo. Wewe una uwezo mkubwa sana wa kufikiri na kutatua matatizo yanayokukabili, jishughulishe tu utaona matokeo yake.
Jioni njema.
Nakuelewa sana kiongozi
 
Heko wadau wa ulingo huu usio na mashabiki wengi.

Siku tatu zilizopita nilienda Mwanza kikazi, ndipo leo muda wa saa 4 au saa 5 asubuhi, tarehe 4 mwezi wa 9, 2018 nimeshuhudia kwa macho yangu msafara wa Raisi wa Tanzania ukikosea njia pale Mwanza kwenye Roundabout iliyoko karibu na BOT MWANZA.
View attachment 856842

Pamoja na kuwa walikuwepo askari wa usalama barabarani lakini nimeshangazwa kuona gari za mbele kusimama ghafla baada ya kuwa zimeingia junction ya Musoma road badala ya kunyooka na Airport road. Baada ya kusimama ghafla gari ya mbele ilipiga honi karibia mara nne, ambapo nafikiri ilimaanisha kutaka msaada wa kuelekezwa njia baada ya kukosea njia sahihi.

Ndipo mmoja wa askari kwenye gari la pili akashuka haraka na kumuonyeshea ishara ya kugeuza ili waendelee na Airport road. Wakati hayo yakiendelea ilibidi msafara wa gari za mbele usimame huku gari za nyuma zikipunguza mwendo kwa ghafla.

Baada ya kushuhudia tukio hilo nikabaki najiuliza maswali mengi, hivi kumbe somo la mawasiliano ni shida hata kwa taasisi nyeti ambazo zinaongoza msafara wa Raisi?


Je mawasiliano ya askari wa usalama barabarani yalikuwa hacked na kupoteza umakini wa taarifa na maelekezo?

Lakini pia nikajiuliza hili tukio kiusalama lina madhara gani?

Karibuni wadau.
WALE JAMAA HUWAGA WANAHARAKA MDA WOTE SOMETIMES HATA MAELEKEZO YA PTAFIKI HAWAYAFUATI, COZ WOA WANAJIONA NDO WENYE NCHI.
 
Alijipiga risasi, alikuwa dogo mmoja hivi fresh from MPA/CCP my village neighbour. Huyu alionewa tu maana alikuwa mgeni na haijui vizuri Bunda (alikuwa ndo kwanza ametoka depo).
Allah amsitiri huko alipo. Huenda hata walimuuwa tu. Unamuua mtu kisa upuuzi huu wa ulimwengu tena mtoto wa maskini bila kuzingatia ana jamaa zake wanamuangalia mtoto wao. Inahuzunisha sana!
 
afrika ni kitu cha kawaida tuuuh
Sio kweli, hapo kuna mtu ataliwa Kichwa kimia kimia mkuu sio kila kitu watu wanatumbuliwa Live. Achilia mbali msafara wa Mhe. RAIS hata msafara wa Mwenge wa Uhuru unakuachisha kazi mchana kweupeeee endapo utaupoteza.
Rmb. Msafara wa Rais Kikwete ulipotea Njia Tarime What happend next?
 
hakuna aliyelalamika hapa mkuu, inaonekana hili jukwaa siyo saizi yako. Ishia kusoma tu comments
Always try to read to understand NOT to read to ask questions,with all my respect to you sijui why umenihukumu kuwa niishie kusoma comments!! wewe ni nani u wants to limit me?inaonyesha umekuzwa kwenye mazingira ya hasira,violent na wazazi wako na matokeo yake ni haya ya kuwa na hasira kiasi hicho,humu kila mtu ana freedom to comments anything but within the Jamii Forums regulations,sio za kwako wewe,na mbaya zaidi hii inaonyesha ni jinsi gani DNA ya hasira inavyosambaa kwa kasi ya ajabu ndani ya nchi yetu,Tanzania tunahitaji ustaarabu wa kila mmoja wetu kuwa huru kimawazo sio kuamuliwa na watu kama wewe,ningekufahamu ningegharimia wewe kwenda kwa wataalam ili wakuchunguze why unaonyesha kuwa ni mtu katili na mwenye hasira.
 
Nimesikia Lissu atakuwa na kongamano tareh 7-9 pengine hili linawachanganya [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom