Msafara wa Raisi (Presidential Motorcade) kukosea njia! Hii imekaaje kiusalama?

Msafara wa Raisi (Presidential Motorcade) kukosea njia! Hii imekaaje kiusalama?

Hilo gari la mawasiliano mmelitengeneza nyie ? Hakuwezi kuwa na bugs ? Hiyo land-line yenyewe mmetengenezewa na wazungu halafu hapa sijui unajisifu nini
Kuna teknolojia nyingi China hajagundua yeye....! Alichofanya China ni ku'reverse engineering'...kwa sasa China anatamba. Sasa, toka mwaka 1961 Tanzania inasomesha mainjinia si China, si US, si EU, si Russia...si Korea...nakadhalika; unategemea wote hao (wengine wako kwenye vyombo vyetu mahususi, kwenye usalama, urainai, n.k.) wameshindwa kuambulia mbinu za ku'chakachua' hizo device kutoka kwa wenzetu waliozigundua? Usiwadharau hivyo wataalamu wetu...kuna mambo mengi wanafanya...ila copyrights zinakuwa za wale waliotoa ufadhiri wakati mwingine.
 
Labda ni ile gari mpya ya mawasiliano iliyopo katika msafara wa Rais wataalam wake hawajaweza ku-master mitambo iliyopo mule. ( Aliyeona msafara wa Rais kwa siku hizi mbili atakubaliana nami )
Ilikuwa kule Taaarime, alijipiga risasi.
 
tupe maelezo mkuu ilikuaje baada ya kukosea na kuelekeza msafara kusiko sahihi?
Nakumbuka ilikua ni ziara mkoani Mara( Tarime kama sikosei) mwanamama akaupoteza msafara wa rais. Kwa mujibu wa taarifa alikamatwa akawekwa ndani ila kesho yake vyombo vya habari viliripoti kuwa amejiua kwa kujipiga risasi. Walisema alichukua bunduki counter akaji tyu tyu..
 
Kuna teknolojia nyingi China hajagundua yeye....! Alichofanya China ni ku'reverse engineering'...kwa sasa China anatamba. Sasa, toka mwaka 1961 Tanzania inasomesha mainjinia si China, si US, si EU, si Russia...si Korea...nakadhalika; unategemea wote hao (wengine wako kwenye vyombo vyetu mahususi, kwenye usalama, urainai, n.k.) wameshindwa kuambulia mbinu za ku'chakachua' hizo device kutoka kwa wenzetu waliozigundua? Usiwadharau hivyo wataalamu wetu...kuna mambo mengi wanafanya...ila copyrights zinakuwa za wale waliotoa ufadhali wakati mwingine.
Ngoja nikiache maana asili ya Mtanzania ni maneno mengi ,huku hamna kitu
 
Asiyepotea/poteza ni Mwenyezi Mungu tu!
 
Walipotea au walikosea hebu badili Kichwa cha Habari
hakuna haja ya kurekebisha kichwa cha thread maana ukweli ni kuwa walikosea njia na kupotea hadi waliposhituka na kurudi njia sahihi, kupotea njia ni matokeo ya kukosea njia.

Hata ukipotea dakika moja bado utakuwa umepotea tu.
 
Kukosea kupo tu ktk maisha ya binadamu, hata hao ambao wapo mbele kwa kila kitu hasa technology pia hukosea mkuu. Alikosea Mungu pia ndio maana kukawepo shetwani.
Mambo ya MUNGU usiyaingize kwenye udhaifu wa kibinadamu mkuu.
 
Nakumbuka ilikua ni ziara mkoani Mara( Tarime kama sikosei) mwanamama akaupoteza msafara wa rais. Kwa mujibu wa taarifa alikamatwa akawekwa ndani ila kesho yake vyombo vya habari viliripoti kuwa amejiua kwa kujipiga risasi. Walisema alichukua bunduki counter akaji tyu tyu..
walimtutu wao wenyewe
 
HAMNA PROTOCOAL ILIYOKOSEWA ILA NI WANA KITENGO WANAMTAFUTIA CHANCE WAMUONDOE KWENYE KITI...KILA MTU KAMCHOKA...HADI MIZIMU. SO HAMNA NAMNA. NA ASIJIDANGANYE AKAPANDA NDEGE...NA MAGARI NDO HIVYO YAMEANZA KUPINDUKA...KAZI ANAYO...
Tuhuma nzito hizi
 
Kweli sisi ni mahodari wa kulalamika kwenye mitandao ,our no 1 kupotea njia ni news wakati kupoteza uelekeo kwa nchi sio news!,tuendelee kusubiri
hakuna aliyelalamika hapa mkuu, inaonekana hili jukwaa siyo saizi yako. Ishia kusoma tu comments
 
Hilo gari la mawasiliano mmelitengeneza nyie ? Hakuwezi kuwa na bugs ? Hiyo land-line yenyewe mmetengenezewa na wazungu halafu hapa sijui unajisifu nini

Kama hizo Satellites za Wazungu ,China nk hamtumii ya kwenu ni ipi mnayo itumia ?

Asalalee!
Hata mimi namshangaa huyo jamaa
 
Heko wadau wa ulingo huu usio na mashabiki wengi.

Siku tatu zilizopita nilienda Mwanza kikazi, ndipo leo muda wa saa 4 au saa 5 asubuhi, tarehe 4 mwezi wa 9, 2018 nimeshuhudia kwa macho yangu msafara wa Raisi wa Tanzania ukikosea njia pale Mwanza kwenye Roundabout iliyoko karibu na BOT MWANZA.
View attachment 856842

Pamoja na kuwa walikuwepo askari wa usalama barabarani lakini nimeshangazwa kuona gari za mbele kusimama ghafla baada ya kuwa zimeingia junction ya Musoma road badala ya kunyooka na Airport road. Baada ya kusimama ghafla gari ya mbele ilipiga honi karibia mara nne, ambapo nafikiri ilimaanisha kutaka msaada wa kuelekezwa njia baada ya kukosea njia sahihi.

Ndipo mmoja wa askari kwenye gari la pili akashuka haraka na kumuonyeshea ishara ya kugeuza ili waendelee na Airport road. Wakati hayo yakiendelea ilibidi msafara wa gari za mbele usimame huku gari za nyuma zikipunguza mwendo kwa ghafla.

Baada ya kushuhudia tukio hilo nikabaki najiuliza maswali mengi, hivi kumbe somo la mawasiliano ni shida hata kwa taasisi nyeti ambazo zinaongoza msafara wa Raisi?

Je mawasiliano ya askari wa usalama barabarani yalikuwa hacked na kupoteza umakini wa taarifa na maelekezo?

Lakini pia nikajiuliza hili tukio kiusalama lina madhara gani?

Karibuni wadau.
mi nafikiri usalama barabarani wa eneo hilo hawa kuwa na taarifa. huwa wanaonesha wapi msafara uelekee.
 
Kwa Tanzania ni kitu cha kawaida kabisa..mbona vingi tu tunavikoseaga!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivo vingine sisi tukikoseaga tunauchuna tunaendelea na safari tu, tena kama muongoza njia mwenyewe kanyamaza basi nasisi tunanyamaza tunakanyaga mafuta mpaka tunamaliza safari, mwisho wa safari ndo unajifanya kushangaa kuwa kumbe tulikuwa rafu rodi kisha unajifanya lakini poa tu maana tumefika salama.
 
hakuna haja ya kurekebisha kichwa cha thread maana ukweli ni kuwa walikosea njia na kupotea hadi waliposhituka na kurudi njia sahihi, kupotea njia ni matokeo ya kukosea njia.

Hata ukipotea dakika moja bado utakuwa umepotea tu.
Ukipotea unatafutwa ukikosea njia unaelekezwa
 
HAMNA PROTOCOAL ILIYOKOSEWA ILA NI WANA KITENGO WANAMTAFUTIA CHANCE WAMUONDOE KWENYE KITI...KILA MTU KAMCHOKA...HADI MIZIMU. SO HAMNA NAMNA. NA ASIJIDANGANYE AKAPANDA NDEGE...NA MAGARI NDO HIVYO YAMEANZA KUPINDUKA...KAZI ANAYO...
Mambo ya kuropoka tu haya unaweza kujikuta matatizoni hata ikakugharimu maisha. Ushauri wangu kuna mambo ya kuyafanyia utani na kuna mambo sio
 
Back
Top Bottom