Msafara wa Raisi (Presidential Motorcade) kukosea njia! Hii imekaaje kiusalama?

Msafara wa Raisi (Presidential Motorcade) kukosea njia! Hii imekaaje kiusalama?

Inaonekana hujui protocol za mambo ya Usalama. Mimi sijamuhukumu ila principles ziko hivyo, hamna namna.
Alijipiga risasi, alikuwa dogo mmoja hivi fresh from MPA/CCP my village neighbour. Huyu alionewa tu maana alikuwa mgeni na haijui vizuri Bunda (alikuwa ndo kwanza ametoka depo).
Kwa mtindo huo mbona askari waliyemwuliza kama ana nia mbaya anaweza kuwaonyeshea njia nyingine na wajipeleka wenyewe kwa maadui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heko wadau wa ulingo huu usio na mashabiki wengi.

Siku tatu zilizopita nilienda Mwanza kikazi, ndipo leo muda wa saa 4 au saa 5 asubuhi, tarehe 4 mwezi wa 9, 2018 nimeshuhudia kwa macho yangu msafara wa Raisi wa Tanzania ukikosea njia pale Mwanza kwenye Roundabout iliyoko karibu na BOT MWANZA.
View attachment 856842

Pamoja na kuwa walikuwepo askari wa usalama barabarani lakini nimeshangazwa kuona gari za mbele kusimama ghafla baada ya kuwa zimeingia junction ya Musoma road badala ya kunyooka na Airport road. Baada ya kusimama ghafla gari ya mbele ilipiga honi karibia mara nne, ambapo nafikiri ilimaanisha kutaka msaada wa kuelekezwa njia baada ya kukosea njia sahihi.

Ndipo mmoja wa askari kwenye gari la pili akashuka haraka na kumuonyeshea ishara ya kugeuza ili waendelee na Airport road. Wakati hayo yakiendelea ilibidi msafara wa gari za mbele usimame huku gari za nyuma zikipunguza mwendo kwa ghafla.

Baada ya kushuhudia tukio hilo nikabaki najiuliza maswali mengi, hivi kumbe somo la mawasiliano ni shida hata kwa taasisi nyeti ambazo zinaongoza msafara wa Raisi?

Je mawasiliano ya askari wa usalama barabarani yalikuwa hacked na kupoteza umakini wa taarifa na maelekezo?

Lakini pia nikajiuliza hili tukio kiusalama lina madhara gani?

Karibuni wadau.
Ni kosa kubwa sana kwa Askari wa usalama barbarani na sio ajabu ukaskia RPC au RTO akawa responsible kwa hilo!
 
Kuna askari mmoja wa kike alipoteza msafara wa Kikwete, yule dada alijinyonga aisee.
Hahaha! Haya maisha bhana, yule manzi aliuwawa aisee.. Hakujiuwa kwa utashi wake, na bado hakuja kuonekana tena kwenye movie ya Prison Break season 5, pamoja na kuwa aliomba msamaha ila akapigwa risasi
 
Ni hatari kwa kweli ukiachana na mawasiliano basi hata ramani wameshindwa Kuwa nayo pia hivi Mishangingi kama ile inakosa TV pale mbele inayoonyesha Ramani!!!....
Sisi baaado sana

'HOW MUCH IS TOO MUCH?'
Yaani unataka miongozo ya misafara ya Rais wetu iongozwe na satellites za US, Russia ama China...!?? Hilo haliwezekani. misafara ya rais wetu tunairatibu sisi...!! Usione zinatumika simu za 'land line' kuna maana yake wakati mwingine.
 
Tatizo ni pale msipoishi nchi zingine na hamuezi kujua ya hizo nchi zingine.yamkini ni jambo la kawaida tu au ni la kupoteza watu kiusalama.huwezi kujua yote kwa kuona kwa macho tu pasi kujua taratibu zao

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumpoteza nani sasa ? Mi nachojua kupoteza watu kiusalama ni pale rais anabadili the usual route basi. Sasa kujidai umebadili afu urudi si ndo kufa sasa

Ngoja nikupe mfano wa ki usalama
Rais wa zaire alikua mara nyingi hafati route za msafara wake yani iaweza kua ilibidi gari zikate kushoto ila yeye anasema ziende kulia na kwenye msafara wake alikua anakaa mbele na hatumii njia moja mara mbili

So u got to admit it kwamba wale mnaowasifiaga sana humu.wamepotea mwanza that means they are not clever at all
Zile gari zina mpaka GPS afu TISS wenu wanapotea

Unakuja hapa unahema umekimbizwa?huelewi nilichosema?nani kakuthibitishia nilichosema ndivyo ilivyo?unakuja na mapovu una kifafa?wewe utabaki na mawazo yako juu ya hilo na mwingine na mfikra zake pia.na wote hatutakua na uhakika na kilichotikea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kukosea kupo tu ktk maisha ya binadamu, hata hao ambao wapo mbele kwa kila kitu hasa technology pia hukosea mkuu. Alikosea Mungu pia ndio maana kukawepo shetwani.
 
Unakuja hapa unahema umekimbizwa?huelewi nilichosema?nani kakuthibitishia nilichosema ndivyo ilivyo?unakuja na mapovu una kifafa?wewe utabaki na mawazo yako juu ya hilo na mwingine na mfikra zake pia.na wote hatutakua na uhakika na kilichotikea

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu. Calm down
Hakuna aliyesema wewe unajua kilichotokea mimi nilichofanya ni kupinga kile ulichokihisi wewe na kuleta changu kwa hoja and that is what JF is so mkuu mimi sina tatizo it was just a normal discussion

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom