Msafara wa Raisi (Presidential Motorcade) kukosea njia! Hii imekaaje kiusalama?

Msafara wa Raisi (Presidential Motorcade) kukosea njia! Hii imekaaje kiusalama?

Heko wadau wa ulingo huu usio na mashabiki wengi.

Siku tatu zilizopita nilienda Mwanza kikazi, ndipo leo muda wa saa 4 au saa 5 asubuhi, tarehe 4 mwezi wa 9, 2018 nimeshuhudia kwa macho yangu msafara wa Raisi wa Tanzania ukikosea njia pale Mwanza kwenye Roundabout iliyoko karibu na BOT MWANZA.
View attachment 856842

Pamoja na kuwa walikuwepo askari wa usalama barabarani lakini nimeshangazwa kuona gari za mbele kusimama ghafla baada ya kuwa zimeingia junction ya Musoma road badala ya kunyooka na Airport road. Baada ya kusimama ghafla gari ya mbele ilipiga honi karibia mara nne, ambapo nafikiri ilimaanisha kutaka msaada wa kuelekezwa njia baada ya kukosea njia sahihi.

Ndipo mmoja wa askari kwenye gari la pili akashuka haraka na kumuonyeshea ishara ya kugeuza ili waendelee na Airport road. Wakati hayo yakiendelea ilibidi msafara wa gari za mbele usimame huku gari za nyuma zikipunguza mwendo kwa ghafla.

Baada ya kushuhudia tukio hilo nikabaki najiuliza maswali mengi, hivi kumbe somo la mawasiliano ni shida hata kwa taasisi nyeti ambazo zinaongoza msafara wa Raisi?


Je mawasiliano ya askari wa usalama barabarani yalikuwa hacked na kupoteza umakini wa taarifa na maelekezo?

Lakini pia nikajiuliza hili tukio kiusalama lina madhara gani?

Karibuni wadau.
Habari za around about mkuu?
 
Labda ni ile gari mpya ya mawasiliano iliyopo katika msafara wa Rais wataalam wake hawajaweza ku-master mitambo iliyopo mule. ( Aliyeona msafara wa Rais kwa siku hizi mbili atakubaliana nami )
Ile gari pana hivi ya kimarekani ina nondo nyingi kwa juu?
 
Who fu@cken care...mimi nahangaika na boda boda kwa safari zangu
 
Huwa
Labda ni ile gari mpya ya mawasiliano iliyopo katika msafara wa Rais wataalam wake hawajaweza ku-master mitambo iliyopo mule. ( Aliyeona msafara wa Rais kwa siku hizi mbili atakubaliana nami )
Huwa ga hukosei unapo reply
 
Back
Top Bottom