Msafara wa Raisi (Presidential Motorcade) kukosea njia! Hii imekaaje kiusalama?

Msafara wa Raisi (Presidential Motorcade) kukosea njia! Hii imekaaje kiusalama?

Labda ni ile gari mpya ya mawasiliano iliyopo katika msafara wa Rais wataalam wake hawajaweza ku-master mitambo iliyopo mule. ( Aliyeona msafara wa Rais kwa siku hizi mbili atakubaliana nami )
Nimepata kitu hapa, kumbe kuna gari mpya ya mawasiliano ilikuwa kwenye msafara mkuu? Inafanyaje kazi hiyo gari?
 
Heko wadau wa ulingo huu usio na mashabiki wengi.

Siku tatu zilizopita nilienda Mwanza kikazi, ndipo leo muda wa saa 4 au saa 5 asubuhi, tarehe 4 mwezi wa 9, 2018 nimeshuhudia kwa macho yangu msafara wa Raisi wa Tanzania ukikosea njia pale Mwanza kwenye Roundabout iliyoko karibu na BOT MWANZA.
View attachment 856842

Pamoja na kuwa walikuwepo askari wa usalama barabarani lakini nimeshangazwa kuona gari za mbele kusimama ghafla baada ya kuwa zimeingia junction ya Musoma road badala ya kunyooka na Airport road. Baada ya kusimama ghafla gari ya mbele ilipiga honi karibia mara nne, ambapo nafikiri ilimaanisha kutaka msaada wa kuelekezwa njia baada ya kukosea njia sahihi.

Ndipo mmoja wa askari kwenye gari la pili akashuka haraka na kumuonyeshea ishara ya kugeuza ili waendelee na Airport road. Wakati hayo yakiendelea ilibidi msafara wa gari za mbele usimame huku gari za nyuma zikipunguza mwendo kwa ghafla.

Baada ya kushuhudia tukio hilo nikabaki najiuliza maswali mengi, hivi kumbe somo la mawasiliano ni shida hata kwa taasisi nyeti ambazo zinaongoza msafara wa Raisi?

Je mawasiliano ya askari wa usalama barabarani yalikuwa hacked na kupoteza umakini wa taarifa na maelekezo?

Lakini pia nikajiuliza hili tukio kiusalama lina madhara gani?

Karibuni wadau.
Lakini wtz bado tume jaa na mawanzo ya kijamaa ....sasa unaona hilo nijambo kumbwa mnapenda sanaa kutukuza vitu....mbona hilo ni kawaida sanaa hata trump wanakosea njia au wanapata emergence nakujirekebisha acha mawanzo ya ujamaa buana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taratibu mkuu, hili ni jukwaa la intelligence, ukiona jambo hili ni la kawaida basi ujue siyo saizi yako, tulia tu usome comments.
 
Tatizo ni pale msipoishi nchi zingine na hamuezi kujua ya hizo nchi zingine.yamkini ni jambo la kawaida tu au ni la kupoteza watu kiusalama.huwezi kujua yote kwa kuona kwa macho tu pasi kujua taratibu zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni pale msipoishi nchi zingine na hamuezi kujua ya hizo nchi zingine.yamkini ni jambo la kawaida tu au ni la kupoteza watu kiusalama.huwezi kujua yote kwa kuona kwa macho tu pasi kujua taratibu zao

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa aina ya reasoning uliyotumia una jumuisha kuwa kila kupotea kwa msafara ni mbinu ya kupoteza watu kiusalama? siyo kila kosa ni mbinu mkuu
 
Back
Top Bottom