Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Ninaangalia matangazo LIVE kupitia luninga za Kenya.
Jambo moja ambalo limenishangaza Sana ni kuona msafara wa Rais mteule, William Ruto, ukienda kwenye kiwanja cha Kasarani, ambako ndiyo kunakotarajiwa kwa shughuli hiyo ya uapisho, akipita barabarani bila kuzifunga barabara hizo, kwa maana nyingine ni kuwa, msafara huo umekuwa ukipishana na magari mengine, yalioko kwenye shughuli nyinginezo!
Nimekuwa nikijaribu ku-imagine, kama shughuli hiyo ingekuwa hapa kwetu Tanzania, barabara ambazo angepita huyo Mheshimiwa, barabara zingefungwa kwa masaa kadhaa na kuathiri shughuli mbalimbali za wananchi hao!
Tumeshuhudia kwa safari za kawaida za Mheshimiwa Rais wa nchi hii, barabara huwa zinfungwa hata kwa zaidi masaa 2, akipishwa Mheshimiwa Rais apite yeye tu na hakuna kubughuziwa na waendesha magari yoyote wengine hapa nchini!
Hebu tujiulize, hivi huu ulinzi wote tunaowapa Hawa viongozi wetu hapa TZ, tafsiri yake ni nini hasa?🥺