Nimepata taarifa rasmi kuwa msafara wa CHADEMA ukiongozwa na Mkiti wao umezuiwa kuingia uwanja wa Taifa kuhudhuria shughuli ya kitaifa kumuaga marehemu Mkapa.
Toka jana nilitambua hili kutokea leo na niliwaeleza baadhi ya watu akiwemo
Innocent Minja.
Hakika chadema hawakuwa na mpango kuhudhuria shughuli hii ya kumuaga Mkapa kitaifa. Uamuzi huu umechagizwa na ombi alilotoa Lissu jana kuomba asindikizwe msibani! Nasema hivyo kwa kuwa kabla ya ujio wa Lissu hakuna hata kiongozi mmoja wa chadema ukiacha Nyalandu aliyeonyesha kuguswa na msiba. Ghafla leo wamekusanyana kwenda msibani kichama!
Kwanza ni ajabu "kualika" watu wakusindikize msibani kichama! Viongozi wa chadema wangeuona upotofu huu palepale Makao Makuu na kuu sahihisha. Wangewahimiza wafuasi waende lakini sio kama kundi la chama. Hivi si kuna CCM, ACT, NCCR, CUF, TLP, CHAUMA n.k.? Viongozi wa chadema wameona wenzao wakivaa uniform za vyama vyao na kuandamana kwenda msibani? Akili hii wao wanaitoa wapi? Kwa Lissu?
Kauli ya Lissu jana kuwa "Mkapa sio raisi wa CCM" ililenga nini kama sio fujo? Lissu aliona CCM peke yao uwanjani? Au alitaka Tu "Dar isimame"? Kutumia msiba kisiasa ni uchawi Sawa kuruka na ungo.
Hivi Mbowe haelewi itifaki? Hajui kiongozi mkuu hufika mwisho na kama kuna milango hufungwa? Alifika mwisho Kwa kuwa anaamini mkuu NI yeye au ujinga Tu?
Mie nasema, Serikali imecheka na kima kuanzia Jana sasa leo kima wametaka kuvamia shamba!
Hawa ilifaa wapate huduma sawa na ya kima kuanzia hiyo Jana. Wanadhani Serikali inawaogopa!