Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wamemaliza sherehe za mapokezi yaLisu?Kwenye post zangu za jana nilishauri Lissu kutokwenda kwenye huo msiba, ninajua vyema mtazamo wa serekali hii chini ya Magufuli dhidi ya Lisu. Hapo tatizo la kuzuiliwa ni Lisu, na kwa vyovyote vile angeingia hapo uwanjani lazima angeshangiliwa vibaya sana, jambo ambalo lingezua fedheha na Karaha kubwa kwa serikali.
Ni nani asiyejua kuwa Lisu na Magufuli kuwa hawaivi chungu kimoja? Hivi hao viongozi wa Cdm walitarajia serikali na ccm, wangekubali cdm wachukue point za mezani mbele yao?
Mkuu sio Kweli ndugu yangu; Watu wananchi wa kawaida huwa wanaingia; Ispokuwa hao ni kwasababu wana eneo maalum na ni upande uleule wa Rais, hivyo itakuwa sio sawa. Nikiwa Kijana nimehudhuria Sherehe za kitaifa, uhuru na Muungano mara kadhaa, Wananchi wanaruhusiwa kuingia na Kutoka bila shida hata kama Mheshimiwa anaendelea Kuhutubia.Kiitikadi Mh Rais akisha ingia mahali gate lina fungwa
Wameshamaliza sherehe za mapokezi ya Lisu?Kumbuka kwamba matukio yote yametokea kwa bahati wakati mmoja. la TL lilipangwa lkn msiba ukatokea. Sasa kwa vyovyote ni busara TL aende kuaga. Kutokufanya hivo ni dharau pia.
Sasa kuhusisha hilo na kuingilia msiba ni jambo lingine na ni mtizamo tu. But kuaga ni muhimu zaidi na pengine ni lazima.
Mnaweza kuwa na chuki na ndugu lakini msiba huwezi kuukwepa
Solution: ni kuwaruhusu with some conditions to avoid disturbance. Otherwise itakuwa ni woga.
Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
Maalimu seifu hana madhara kwa ccm. Huwezi kujua, CHADEMA sio wajinga kivile. Huwenda walifanya mawasiliano lakini wakapuuzwa. You never know, ccm wana hila usijifanye huwajui.
Msafara wa Viongozi Wakuu wa CHADEMA, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Freeman Mbowe, wamezuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru walikokuwa wameenda kuhudhuria shughuli ya kutoa heshima za mwisho na kumuaga Rais Mstaafu wa Awamu Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa.
Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Mbowe aliongozana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa (Bara), Mhe. Tundu Lissu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mhe. John Mnyika, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee, Mhe. Hashim Juma Issa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama, Mhe. Suzan Kiwanga na viongozi wengine waandamizi kutoka Makao Makuu ya CHADEMA, Viongozi wa Kanda 10 za chama, Viongozi CHADEMAwa Mikoa, Wilaya na Majimbo mbalimbali nchi nzima.
View attachment 1519379
Kutoka Uwanja wa Uhuru hapa, Dar es Salaam.
Mbona kama vile mtabiri wa nyota! Kwamba ni heri wazuiwe wasiingie kabisa, kuliko waingie halafu wanung'unike kuwekwa kwa wananchi! Haya bhana, mi napita tuNa wangeachwa wakakae kwa wananchi wa kawaida kungeleta MANUNGUNIKO kwa jamii kama wametengwa na tungeamini hivyo mkuu.
Wamemaliza sherehe za mapokezi yaLisu?
Kama umechukia pasukaa! Who are you? Toa ushauri ccm na wanaovunja katiba! Ukishindwa kula mihogo!Kuwa kiongozi mkubwa ni pamoja na kuwa na nidhamu , kwa hili Chadema wamekosa nidhamu..Nia yao wakazue taharuki tu kwenye msiba mbele ya Rais na wageni wake.
Acheni kiki zenu za kitoto, pangeni mipango ya maana kuelekea Uchaguzi mkuu sio sifa za Kijinga.
Duh! Kama nyie ndio wafuasi mnaotegemewa CDM, na unajibu hivi!! No wonder chama kinakufaMagufuli si anakubalika? Watanzania wasingekuwa na time na Lissu maana wana Magufuli wao hivyo wangetulia tuu viongozi wa Chadema wajipitie zao wakaketi majukwaani. HAHAHAHAHA jana mlikuwa nma test zali eti kama Chadema inakubalika mlipotoka kapa mmeanza tena uhuni.
Halafu uelewe kuwa Chadema hawakuwa na barua ya mualiko, pale ni msibani. Pia Chadema hawana king'ora hivyo wangejipitia tu barabarani wawahi. Pia elewa msafara ule ulikuwa ni wa viongozi watupu tena wasio na bendera za chama. Mbona maccm yamejazana majukwaani na mijezi yao?
Haya kila mtu afanye tukio lake. Kazikeni mtu wenu salama sisi tuendelee na yetu! Utadhani maiti zinaliwa kwamba Chadema wakiwepo nyama itapungua! Ushenzi kabisa.
Narudia tena "Msiba hauna mualiko wala kadi za michango"
Huo ni msiba na hauna/hautakiwi kuwa na mashariti ya aina hiyo.Kama wamefika hapo baada ya Rais kuingia hawawezi kuruhusiwa. Au wameenda na 'maandamano' msibani?
Huu haukuwa Msiba wa kawaida, Leo ilikuwa shughuli maalumu ndio maana itifaki zote zimefuatwa..Magufuli si anakubalika? Watanzania wasingekuwa na time na Lissu maana wana Magufuli wao hivyo wangetulia tuu viongozi wa Chadema wajipitie zao wakaketi majukwaani. HAHAHAHAHA jana mlikuwa nma test zali eti kama Chadema inakubalika mlipotoka kapa mmeanza tena uhuni.
Halafu uelewe kuwa Chadema hawakuwa na barua ya mualiko, pale ni msibani. Pia Chadema hawana king'ora hivyo wangejipitia tu barabarani wawahi. Pia elewa msafara ule ulikuwa ni wa viongozi watupu tena wasio na bendera za chama. Mbona maccm yamejazana majukwaani na mijezi yao?
Haya kila mtu afanye tukio lake. Kazikeni mtu wenu salama sisi tuendelee na yetu! Utadhani maiti zinaliwa kwamba Chadema wakiwepo nyama itapungua! Ushenzi kabisa.
Narudia tena "Msiba hauna mualiko wala kadi za michango"