Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Na hawa watu wanaoingia mudahuu ni maraisi wa wapi?
 
Walifika baada ya Mhe. Rais kufika au? kama walikuta Rais ameshafika basi ni halali wazuiwe.
 
Hawa jamaa wanafanya mzaha na msiba wa taifa . Kiki ya jana imebuma wameona waende wakatafute kiki nyingine msibani. Aibu sana kwa CHADEMA.
Kumbuka kwamba matukio yote yametokea kwa bahati wakati mmoja. la TL lilipangwa lkn msiba ukatokea. Sasa kwa vyovyote ni busara TL aende kuaga. Kutokufanya hivo ni dharau pia.

Sasa kuhusisha hilo na kuingilia msiba ni jambo lingine na ni mtizamo tu. But kuaga ni muhimu zaidi na pengine ni lazima.

Mnaweza kuwa na chuki na ndugu lakini msiba huwezi kuukwepa
Solution: ni kuwaruhusu with some conditions to avoid disturbance. Otherwise itakuwa ni woga.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Hatuwezi kukubali chadema wanajisi msiba wa marehemu mzee wetu mkapa, nchi hii ina intelijensia kali ambayo tulifahamu kwa muda mrefu kwamba hawa watu wanataka kunajisi msiba.

Siasa za matukio zimepitwa na wakati.
 
Kuna Watu ninawashauri kwa nia njema tu kuwa wawe makini mno kwani kuna Mtu namuona anahutubia ila ana Hasira na Kisununu sana Moyoni.

Uko sahihi mkuu, ile hali ya jana huyo mkuu wa itifaki hapo, sio mvumilivu wa hali ile. Na sijui kwanini viongozi wa Chadema hawajifunzi tabia ya mtu. Kuna mbinu nyingi za kushindana na mtu wa aina hiyo, na bado ukammudu kuliko kutengeneza taswira ya mivutano.
 
Siasa tu mpaka kwenye Misiba?

Hapo serikari yote iko hapo, Maana yake kuna ulinzi na Interejensia ya kutosha, kina Tundu na Chadema wao wanaamua kwenda kujitangaza Kisiasa kwenye Jambo la simanzi?

Hata kama siasa ndio zinatupangia Kwa kila ktu Ila si kwenye Msiba
 
Walikuwa wapi mpaka waingie wakati Rais ameshaingia ndani? Itifaki lazima izingatiwe.
Mkuu, kwani hakuna wengine wameendelea kuingia baada ya raisi? Pia rais njia ni nyeupe wengine kuna foleni na ukumbuke mtu alifika jana tu na uchovu wa safari na kusema kweli lazima maandalizi yawepo kutokana na yaliyotokea huko nyuma.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…