Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Mwanahabari Huru,

Mimi nashauri wasiwazuie. Walitakiwa wawazuie kama wangeenda kwa namna ya maandamano ambayo yangeonyesha kuwa wanataka kuutumia msiba wa wa-Tanzania kama kick ya kisiasa.

Hawa watu kwa sababu ni Viongozi na ni wamoja na wameamua katika umoja wao kuhudhuria kwa staili, waachwe. Kwa mfano Tundu Lissu jana kama wangezuia msafara wa wafuasi wake kumpokea airport.

Ujio wake ungekuwa na impact kubwa zaidi kuliko ilivyotokea jana, lakini walivyomu-ignore, wala hapajatokea chochote kile chenye impact kubwa sana.

Mwaka 1995 kwenye kampeni, Mrema alikuwa anabebwa na wafuasi wake, halafu kukatokea mamlaka zikawa zinazuia asibebwe.

Ilipofika siku ya uzinduzi wa Kampeni za CCM jangwani, Mwalimu Nyerere akauliza swali, mtu anayebebwa anavunja sheria gani ya JMT?
 
Wamekwenda muda gani? Wamekwenda baada ya kuingia Rais au baada ya kuingia Rais?

Viongozi wote isipokuwa Rais kiutaratibu huingia kabla ya kiongozi mkuu wa nchi hajaingia!

Mtu wa mwisho anaye ingia kwenye tukio lolote la kitaifa huwa ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania!

Hebu Twambie wao wametaka kuingia muda gani? Wakati Rais kuingia au kabla?
Hivi kweli mko serious mnataka kwenda ikulu? Hamkujua ratiba?
Wameingia kabla
 
Wamekwenda muda gani? Wamekwenda baada ya kuingia Rais au baada ya kuingia Rais?

Viongozi wote isipokuwa Rais kiutaratibu huingia kabla ya kiongozi mkuu wa nchi hajaingia!

Mtu wa mwisho anaye ingia kwenye tukio lolote la kitaifa huwa ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania!

Hebu Twambie wao wametaka kuingia muda gani? Wakati Rais kuingia au kabla?
Hivi kweli mko serious mnataka kwenda ikulu? Hamkujua ratiba?
Unauliza kwa kuwa hujui na mwisho unaishia kulaumu, am sorry for you.
 
Kuna Watu ninawashangaa mno Mkuu kwani wanamjua kabisa Mwamba alivyo na Kisununu na Kisasi na Wao wanaendelea Kumtibua tu kama hivi.

Hisia na mapenzi yasitufanye tushindwe kupima matokeo ya maamuzi yetu. Bado kuna uwanja na nafasi ya kutosha ya kiushindani, kuliko kutengeneza image isiyo na faida kwa yoyote, kwenye hafla hiyo.
 
Labda wanaangalia utaratibu jinsi ya kuwapanga, nani akae wapi na nani akae wapi.
Umewaza kama Mimi. Zaidi kama hawajawasiliana kabla na wahusika,lazima pawe na shida kidogo, hata usalama wao pia wapaswa kuwa wa upekee fulani.
 
Hivi na wewe upo Jf lakini hujui kuna utaratibu wa kuingia kwenye sherehe za kitaifa? Hujui kuwa Rais ndio huwa wa mwisho kuingia?
Nadhani wangeruhusuliwa kuingia ila waambiwe wakakae jukwaa la waombolezaji wa kawaida.
 
Pengine walienda na magari yenye bendera za chama.
 
Kwa hiyo aliekufa sio mtu? Yaani MATAGA akili hamnazo kabisa
Unafikiri Mkapa kama Mawazo?

Kama waliwahi sawa ila kama walichelewa baada ya mkuu wa nchi ilo kosa lao,maana wale lazima wakae sio majukwaa ya watu wa kawaida lazima wangekaa kwenye mahasusi kwa viongozi maarufu.

Ila ukilichukukia kisiasa sawa.
 
Watu wanapiga kelele humu hawajui hata mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa idara wameenda na Coaster maalum 😁😁😁

Hapo ndani kuna protocal za magari ya kina nani yanaruhusiwa kuingia hapo ndani

Tuache masihara!

Uko sahihi, na kwa aina ya ulinzi uliopo hapo, kwa maamuzi ya busara tu unaweza kupima upi utakuwa muongozo.
 
Tunazuiana mpaka kwenye misiba. ukienda tatizo usipoenda ndo kabisa
Wasingeenda tu, maana hata Magufuli huwa haendi kwenye misiba mbalimbali ambayo watz wamepoteza maisha kwa idadi kubwa, mfano wale wa tetemeko la Kagera au kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere.
 
Back
Top Bottom