Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Serikali ilitoa utaratibu wa viongozi wote kuingia uwanjani. Waliambiwa magari yao wakayapaki Karimjee na wangeondoka kwenye msafara mmoja kwa kutumia magari yaliyoandaliwa.

Lakini kwa kuwa CHADEMA wana hobby ya kukiuka taratibu zilizopangwa ili kusababisha taharuki, kujenga picha kuwa wanabaguliwa na pia kujipatia kiki, wanafanya hivi kwa makusudi.
 
Sikubaliani na hili kabisa huu msiba Ni wa Taifa na Wala siyo wa chama.

Let all people to condolence thier former president bila kujali itikadi zao.
 
Serikali ilitoa utaratibu wa viongozi wote kuingia uwanjani.. Waliambiwa magari yao wakayapaki Karimjee na wangeondoka kwenye msafara mmoja kwa kutumia magari yaliyoandaliwa. Lakini kwa kuwa CHADEMAwana hobby ya kukiuka taratibu zilizopangwa ili kusababisha taharuki, kujenga picha kuwa wanabaguliwa na pia kujipatia kiki, wanafanya hivi kwa makusudi.
Kwa hiyo wamezuiwa kwa kuwa walienda kwa gari? Na wasio na magari je, wakapaki nini Karimjee?
 
Wasingeenda tu, maana hata Magufuli huwa haendi kwenye misiba mbalimbali ambayo watz wamepoteza maisha kwa idadi kubwa, mfano wale wa tetemeko la Kagera au kuzama kwa kivuko cha mv nyerere.

Jana nilishauri hilo, na hasa nilishauri Lisu kutokwenda kwenye huo msiba. Huo msiba unaweza kuzua hisia hasi dhidi ya cdm, na ccm/serikali kuamua kuchukua hatua mbaya dhidi ya cdm. Usimpe adui yako nafasi rahisi ya kupambana na ww.
 
Chadema wajinga wajinga hao. Kwanini wazuiliwe bhana.😅😅
CDM ni marehemu mtarajiwa
 
Namuona Maalim Seif katulia hapo itakuwa ndiyo mwakilishi wao.

Hao jamaa wanajipangia ratiba yao as if wanaenda kwenye msiba wa mbwa wa Nasari.😁
 
Mwanahabari Huru,

Lissu alipoomba watu wajitokeze uwanja wa taifa kwenda kumuaga rais Mkapa, watu walitaka kujua muda, na yeye aliwajibu vizuri kwamba katika hili yeye ni mgeni hivyo wenyeji wake (viongozi) watafanya utaratibu ni kutoa mwongozo.
Lilikuwa ni jukumu la uongozi wa juu wa CHADEMA kuwasiliana na serikali ili wapate utaratibu na muda wa kuingia. Ieleweke, leo ni siku ya mwisho kuuaga mwili wa mpendwa wetu.

Hivyo basi, viongozi wote wa juu wa nchi wakiongozwa mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wangekuwa uwanjani, kitendo cha uongozi wa juu wa nchi kuwepo uwanjani ni lazima itifaki za uingiaji zizingatiwe, haiwezekani waje kuingia wakati viongozi wote wameshaingia.

Kama CHADEMA walijiibukia tu tena wakiwa na Makundi wakati viongozi wameshaingia ilikua ni sahihi kabisa kwao kuzuiliwa.

Katika hili nawashauri CHADEMA, badala ya kulalamika na kutaka kutengeneza mapichapicha waombe ladhi. Walipaswa kushirikiana badala ya kujiamulia.
 
Nikweli watu wangelianza kusema Rais! Rais! Rais! Rais!

Tena wangekuwa wanatamka neno hilo kwa mzuka na hamasa kubwa. Nina hakika isingekuwa msiba tena, bali ingekuwa tambo za kisiasa za cdm na ccm. Kama kweli viongozi wa Cdm walitaka kwenda msibani, walipaswa kuchukua utaratibu toka jana, kisha wajipange kuendana na utaratibu uliopo. Japo kwangu busara kubwa ilikuwa ni kutokwenda, hasa hasa Lisu.
 
Civilisation imewapitia mbali sana MATAGA!

Usishangae wakaambiwa wameandamana bila Kibali.

Ubaguzi huu sasa unahamia mpaka kwenye misiba na ipo siku utakwenda zaidi ya hapo.

Ya jana yamewaumiza, na hizi ndio hasira zao.

Hatari ya uamuzi huu ni msiba kuchukua sura ya kisiasa na matokeo yake watu wanaweza kususa kushiriki ikiwamo kuondoka msibani kwa waliokwisha kufika.

Ila kama kuna sababu ya msingi ya kuwazuia,tuambiwe.
Mmeshindwa kuacha sherehe yenu ya mapokezi jana, mmekesha mnakunywa Ma Faru John na mmesakata rhumba mpaka machweo, leo ndio mvae ma T-shirts yenu kuja kuuza sura uwanjani napo mu enjoy mwili wa mpendwa wetu!! kwendaaa! mngekua na uchungu msingefanya sherehe jana na mbwembwe mitaani, tuacheni tuomboleze nendeni mkagonge faru john zenu huko.
 
Kuna Watu ninawashauri kwa nia njema tu kuwa wawe makini mno kwani kuna Mtu namuona anahutubia ila ana Hasira na Kisununu sana Moyoni.
Atapasuka mwaka huu, anataka kutuendesha Watanzania wote kama anavyofanya kwa mke na watoto wake nyumbani, haiwezekani.
 
Back
Top Bottom