Msaga Sumu amshukia vikali Fid Q, asema atafute kazi ya kufanya, aache roho mbaya

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Mfalme wa singeli nchini Tanzania, Msaga Sumu amefunguka na kumtaka rapa Fid Q akae kimya kama alivyofanya mwenzake Afande Sele kuliko kuonesha wivu na roho mbaya yake katika kuzungumzia vitu ambavyo havijui undani wake.

Msaga Sumu ameeleza hayo katika kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kusikia kauli ya Fid Q ilikuwa inadai utunzi wa nyimbo za singeli umekaa kihuni na usela mwingi jambo ambalo kwa mtazamo wake anahisi anarudishwa nyuma katika ile miaka ya muziki kuonekana hauna maana ni uhuni mtupu kwa jamii.

"Ungekuwa muziki wa kihuni inamaana hata serikali ingeingilia kati suala hilo, chamsingi mtu anatakiwa akaushe tu kuongelea mambo mengine. Haya ni maisha na huu ni muziki kama anavyoona mingine tena muziki huu unaweza kuwa bora kuliko ambao wao wanaofanya. Singeli inapendwa na kila rika", amesema Msaga Sumu.

Pamoja na hayo, Msaga Sumu ameendelea kwa kusema "yeye kama hana mambo ya kufanya akaushe kama mwenzake Afande sele. Fid Q ndio mtu wa kwanza namsikia kusema muziki huu ni wakihuni tokea nazaliwa huu ni wivu na roho mbaya kwa sababu hakuna mtu yeyote aliyewahi kuzungumzia hii roho mbaya lakini labda nimwambie tu amechelewa".

Mtazame hapa chini Msaga Sumu na Fid Q wakifunguka mengine zaidi.

Kwakweli ata uchezaji wake una walakini.watoto wa kiume wanabidua kiuno na kutikisa matako utasema wa kike.
Uchezaji wake unanitia nyongo mm,especially akicheza mtoto wa kiume

Fid q kasema kweli iliyotukuka
 
Kweli mzee kuna nyimbo niliisikia wanasema" shika ukuta mwanangu tucheze singeli" sasa mwanaume anashikishwa ukuta acheze singeli mziki huu umejaa uhuni mtupu
 
Extremely bad aspecial dancing style. Fid is right.
wamama wavua nguo mbele ya watoto sababu ya huu muziki mitaani.
BASATA WANGECHUKUA TU HATUA STAHIKI ASEE.
 
Tatizo wengi wetu tukiambiwa ukweli tunachukia,ona sasa Msaga Sumu anamwambia Fid Q ana roho mbaya wakati jamaa kasema ukweli.
Jina lenyewe tu Msaga Sumu linasadifu maneno ya Fid Q.
Namshangaa Prof J eti nae kaimba singeli khaaa.
 
Mdundiko-mnanda-mchiriku-kibaokata-Singeli huu ni utamaduni wa Mtu wa pwani hauwezi kuuawa....
 
Singeli ni muziki wa Pwani. Faridi Kubanda is free to share his opinion but it doesn't mean he's right in everything. Ninavyofahamu mimi, huwezi kumpangia msanii jinsi ya kuwakilisha sanaa yake kwa hadhira. Take it or leave it, sio watu wote tunapenda michoro ya Picasso japo ni maarufu Duniani. Kuna visa vingi vilitokea huko nyuma kwavile wasanii walitakiwa wafanye kazi zao kwa matakwa ya watu flani. Hii ni habari kubwa, Fid Q hajui kitu
 
Mfalme wa singeli nchini Tanzania, Msaga Sumu amefunguka na kumtaka rapa Fid Q akae kimya kama alivyofanya mwenzake Afande Sele kuliko kuonesha wivu na roho mbaya yake katika kuzungumzia vitu ambavyo havijui undani wake.

Msaga Sumu ameeleza hayo katika kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kusikia kauli ya Fid Q ilikuwa inadai utunzi wa nyimbo za singeli umekaa kihuni na usela mwingi jambo ambalo kwa mtazamo wake anahisi anarudishwa nyuma katika ile miaka ya muziki kuonekana hauna maana ni uhuni mtupu kwa jamii.

"Ungekuwa muziki wa kihuni inamaana hata serikali ingeingilia kati suala hilo, chamsingi mtu anatakiwa akaushe tu kuongelea mambo mengine. Haya ni maisha na huu ni muziki kama anavyoona mingine tena muziki huu unaweza kuwa bora kuliko ambao wao wanaofanya. Singeli inapendwa na kila rika", amesema Msaga Sumu.

Pamoja na hayo, Msaga Sumu ameendelea kwa kusema "yeye kama hana mambo ya kufanya akaushe kama mwenzake Afande sele. Fid Q ndio mtu wa kwanza namsikia kusema muziki huu ni wakihuni tokea nazaliwa huu ni wivu na roho mbaya kwa sababu hakuna mtu yeyote aliyewahi kuzungumzia hii roho mbaya lakini labda nimwambie tu amechelewa".

Mtazame hapa chini Msaga Sumu na Fid Q wakifunguka mengine zaidi.

Msaga Sumu ni miongoni mwa mazuzu mahiri hapa mjini
 
Et hainaga ushemeji....
Nn Kama sio ufala alafu MTU anadai sio mziki wa kihuni
 
Tatizo wengi wetu tukiambiwa ukweli tunachukia,ona sasa Msaga Sumu anamwambia Fid Q ana roho mbaya wakati jamaa kasema ukweli.
Jina lenyewe tu Msaga Sumu linasadifu maneno ya Fid Q.
Namshangaa Prof J eti nae kaimba singeli khaaa.

Prof J ametukana kwenye hayo mashairi yake aliyoimba juu ya mdundo wa singeli??
 
Singeli ni muziki wa Pwani. Faridi Kubanda is free to share his opinion but it doesn't mean he's right in everything. Ninavyofahamu mimi, huwezi kumpangia msanii jinsi ya kuwakilisha sanaa yake kwa hadhira. Take it or leave it, sio watu wote tunapenda michoro ya Picasso japo ni maarufu Duniani. Kuna visa vingi vilitokea huko nyuma kwavile wasanii walitakiwa wafanye kazi zao kwa matakwa ya watu flani. Hii ni habari kubwa, Fid Q hajui kitu
Anyway you try putting it.. Singeli hii sio uramaduni tena ni uhuni na ujinga.. Hakuna inachoelimisha hakuna inchohifadhi.. Wakiwaachia akina msagasumu na ujinga wanaofanya..kama utamaduni utageuka na kufa kama ilivyokuwa kwa Taarabu.
 
[QUOTEabuu bin umar seydun, post: 26074354, member: 409132"]Kweli mzee kuna nyimbo niliisikia wanasema" shika ukuta mwanangu tucheze singeli" sasa mwanaume anashikishwa ukuta acheze singeli mziki huu umejaa uhuni mtupu[/QUOTE]
Yaaan af ndo style yao pendwa ya kuucheza huo mziki,wakikosa ukuta wa kushika unakuta wameikumbatia ardhi,hadi mitoto ya kiume inacheza imeshika chini.
 
Kwa mala ya kwanza namsikia mtu mzima farid kubaaa kwenye polojo za wahuni wa mtaa.
 
kuna nyimbo tukizisikiliza wengine tunahisi seli za ubongo zafa!!
 
Back
Top Bottom