Uchaguzi 2020 Msajili aonya mpango wa vyama kuungana Oktoba 3

Uchaguzi 2020 Msajili aonya mpango wa vyama kuungana Oktoba 3

Hivi hii ofisi inafanya nini exactly?

Serikali ina ajira za ajabu sana
 
Msajili acha kuchachawa!! Mambo mbona bado kabisa haya!!
 
Kama kuhadaa wananchi ni kosa basi CCM ingekuwa imeshafutwa tongea zamani. Msajili akumbuke raia zikifunguliwa ziingie barabarani atakuwa kwenye wakati mgumu zaidi, cha kufanya sasa hivi aache waungane na sisi tutaamua wenyewe zipi mbivu zipi mbichi kwenye sanduku la kura.
 
Wananchi wanaruhusiwa kusikia,kuona na kuhudhuria mikutano ya wagombea,
Upigaji kura na kuchagua,ni SIRI YA MPIGA KURA
Ni wapi mwananchi (mpiga kura atachanganywa).
 
Woga wa
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini Sisty Nyahoza, ameviasa vyama vya siasa vinavyotaka kuungana siku ya Oktoba 3 mwaka huu, kuacha mara moja mpango huo kwani wanakiuka utaratibu wa sheria na kwamba walianza vizuri hivyo ni vyema kila mmoja akaendelea kunadi sera zake.

Nyahoza ametoa kauli hiyo hii leo Oktoba Mosi, 2020, kwenye kipindi cha Supa Breakfast ya East Africa Radio na kuongeza kuwa hata hivyo tayari Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imekwishaviandikia barua vyama hivyo kwa kuwa ni masuala ya kiofisi huwa hawaziweki barua hizo hadharani.

"Kwanza tunaawaasa hao wanaotaka kufanya hivyo tarehe 3 sisi kama walezi wa vyama vya siasa kwa sababu wanakiuka sheria, walianza vizuri hivyo kila mmoja aendelee kunadi sera yake na wagombea wao wa urais", alisema Nyahoza.

Amesema sheria ya vyama vya siasa inawekwa kwa maslahi ya wanachama na wananchi na unapotaka kushirikiana hutakiwi kufanya kitendo chochote kinachohadaa wananchi kwa hiyo ni kosa kufanya hivyo ghafla wakati wa uchaguzi.

“Ukiunganisha nguvu na chama kingine wakati mmeshakubaliana na wananchi kwamba mtatekeleza sera gani ni kuwahadaa, sisi tulishawasiliana nao na tukawaambia waache," alisema Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini Nyahoza.

Vyama vya siasa vya upinzani vya ACT-Wazalendo na Chama Cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema) vimekuwa vikitajwa kuwa na mpango wa kumuunga mkono mgombea mmoja wa urais Oktoba 3, licha ya kuwa vyama vyote hivyo vimeshasimamisha wagombea wao wa urais.
Woga wa nini? Maana ya kuungana vitu viwili au zaidi kuwa kimoja mfano TANU na AFRO SHIRAZI vilipoungana na kuwa CCM lakini 3 October ni makubaliano ya kwenda pamoja huku kila chama kikibaki kama kilivyo
 
Hwaungani wala kuunganisha vyama bali wanaungana mkono! Jambo hili si lazima liambatane na kubadili sera au kuanza kunadi sera ya chama kingine , wanaweza kuendelea sera zao kila chama na papohapo wakawashawishi wananchi kumchagua mgombea yupi! Hivi vyama vyote vya upinzani vina sera zinazoelekeana so haina kufeli ni complications tu msajili! Mbona haongelei vyama vinavyounga mkono ccm????
 
Naona kama ndio anauhabarisha umma tukajazane kushuhudia maana wengine tulikua hatujui nini kinaenda kutendeka october3
 
Back
Top Bottom