Pre GE2025 Msajili apiga Marufuku Kongamano la CHADEMA mkoani Mbeya, asema matamko yao yanahusisha vitendo vya uvunjifu wa amani

Pre GE2025 Msajili apiga Marufuku Kongamano la CHADEMA mkoani Mbeya, asema matamko yao yanahusisha vitendo vya uvunjifu wa amani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
View attachment 3066772
Msajili wa vyama vya Siasa amepiga Marufuku Kongamano la Chadema mkoani Mbeya lililokuwa kifanyike kesho Jumatatu

Msajili amesema matamko ya Chadema yanaashiria uvunjifu wa Amani. Amesema kwa mfano Bavicha wanasema " Siku hiyo tutaweka hatma ya nchi yetu Tanzania kama ambavyo Vijana wa Kenya Gen Z wamejitambua tunaenda kuweka Maazimio makubwa ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi mkuu wa 2025"

Kwahiyo Ili kulinda Usalama wa Raia na Mali zao Msajili wa Vyama vya Siasa amefutilia mbali Kongamano hilo

Source: Mwananchi

Pia soma=> Jeshi la Polisi lapiga marufuku mkutano wa BAVICHA siku ya vijana duniani
Hayo mamlaka kayapata kutoka sheria gani? Mtoa Mada, tafadhari tuhabarishe vipengere vya sheria au katiba alivyotaja ktk maamuzi hayo…
 

Msajili wa vyama vya Siasa amepiga Marufuku Kongamano la Chadema mkoani Mbeya lililokuwa kifanyike kesho Jumatatu.

Msajili amesema matamko ya Chadema yanaashiria uvunjifu wa Amani. Amesema kwa mfano Bavicha wanasema " Siku hiyo tutaweka hatma ya nchi yetu Tanzania kama ambavyo Vijana wa Kenya Gen Z wamejitambua tunaenda kuweka Maazimio makubwa ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi mkuu wa 2025".

Kwahiyo Ili kulinda Usalama wa Raia na Mali zao Msajili wa Vyama vya Siasa amefutilia mbali Kongamano hilo.

Source: Mwananchi

Pia soma=> Jeshi la Polisi lapiga marufuku mkutano wa BAVICHA siku ya vijana duniani
Msajili hataki mkutano wa kuweka mikakati ya chaguzi za serikali za mitaa kwa Chadema huku Nchimbi na Makalla wakifuatana na saliti Masigwa wanafanya kampeni nchi nzima 😡
 
Wangewaacha tu...

Kuwazuia ni kuwapa mileage ambayo hawana...
Tena pamoja na kuwaongezea wafuasi. Hawa watu ama hawapewi taarifa sahihi na vyombo vya usalama ama wanajiamulia tu kwa mawazo yao.
Rais Samia tumbua hawa inaonekana hawajaelewa 4Rs.
 
..Chura kiziwi / Polisi / Msajili wangepotezea tu kama walivyopotezea kwenye maandamano.

..Hii habari ya kuogopa na hofu ndiyo inasababisha mambo ya kijinga kama tukio la Sativa.
Hapa wanaenda kumpa Mwabukusi sifa nyingine.
 
Ni aibu kubwa sana kwanini asifute upinzani tubaki na sisiemu tubanane humohumo chama kimoja. ? Mnajinasibu kufanya makubwa halafu how come mnaogopa hawa CDM kulikoni?
CCM bila mbeleko ya Polisi, ni wepesi kukiko tissue!😀
 
Nisaidieni, kifungu kipi cha sheria kinampa mamlaka msajili wa vyama kupiga marufuku mikutano? Au ni kuvimbiwa tu?
 
Back
Top Bottom