Thubutu! Kuna taasisi ukiweka mishahara midogo (ya kawaida) utakuwa umepalilia rushwa na wizi utakaopelekea uchumi ku collapse. Mfano afisa wa TRA anayeenda kumkadiria mfanyabishara kodi ya mamilioni au bilioni umlipe milioni moja au mshahara sawa na mwalimu au afisa maendeleo au bwana kilimo!
Hii statement ilipenda kutolewa na viongozi wa kisiasa wa miaka ya 90 huko wasiopenda kuwajibika katika madhambi yao na ili tu kulinda maslahi yao binafsi.
Lakini kiuhalisia huyo mfanyakazi wa TRA anapoishi na kufanya kazi kwenye mazingira wezeshi na rafiki, hawezi kuteteleka na rushwa vinginevyo huyo mtu ni mshenzi na mrafi tangu kuzaliwa kwake.
Mfano mdogo
1) Unanilipa laki 3 tu kwa mwezi lakini sehemu Nzuri ya kuishi, chakula kizuri, huduma za kibinaadam za msingi zipo zote, usafiri upo Kama unahitajika na kila nikikuhitaji kwa msaada wowote ule unanifikia kwa haraka bila ukiritimba, pia ufisadi na mafisadi wanawajibika na kuwajibishwa ipasavyo, Amani imetawala…
Vs
2) Unanilipa mshahara milioni 3, huduma za maisha za msingi mbovu, chakula, makazi, usafiri, miundo mbinu, vyote vya hovyo na ufisadi na mafisadi wanapambwa badala ya kuadhibiwa, rushwa na ukiritimba ndio PGO ya utendaji, Amani ya mashaka mashaka…
Unadhani situation namba ngapi itanisukuma kupokea rushwa kwa haraka zaidi?