Uchaguzi 2020 Msajili: Mgombea aliyesema ataingiza watu barabarani kama akishindwa Urais ametoa lugha za vitisho, siyo ustaarabu

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Msajili msaidizi wa Vyama vya Siasa mh Nyahuza amevitaka vyama vya upinzani kuacha mbwembwe na kuzingatia sheria tunapoelekea uchaguzi mkuu.

Nyahuza amesema kuna mgombea urais ametoa vitisho vya kuingiza watu barabarani endapo atafeli kwenye uchaguzi wa Rais, mtu huyo amepungukiwa ustaarabu.

Pia soma> Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu: Nikiibiwa kura nitawaingiza wananchi barabarani

Maendeleo hayana vyama!
 
Mbona anachukua sentensi nusu nusu ameacha kisababishi, Lissu alisema 'endapo ataibiwa kura' ataingiza watu barabarani, mbona iko wazi hata Seif kasema hivyo hivyo.

Ila angalau meseji zimeanza kuwafikia walizoea watu wa kuwaambia tutamwachia Mungu, Lissu ni mgombea sahihi kwa muda sahihi.
 
Nyahuza amesema kuna mgombea urais ametoa vitisho vya kuingiza watu barabarani endapo atafeli kwenye uchaguzi wa Rais, mtu huyo amepungukiwa ustaarabu.
Hapo hakusema endapo atafeli, bali endapo ataibiwa kura. Msajili angenukuu vizuri, halafu aseme kama atakayeiba kura amepungukiwa au hajapungukiwa ustaarabu
 
Msajili msaidizi wa vyama vya siasa mh Nyahuza amevitaka vyama vya upinzani kuacha mbwembwe na kuzingatia sheria tunapoelekea uchaguzi mkuu.

Nyahuza amesema kuna mgombea urais ametoa vitisho vya kuingiza watu barabarani endapo atafeli kwenye uchaguzi wa Rais, mtu huyo amepungukiwa ustaarabu.

Maendeleo hayana vyama!

Amekosea huyo msajili, Lisu amesema iwapo atashindwa kwa kuporwa ushindi hatamuachia Mungu. Na iwapo ushindi utakuwa ni huu wa kishenzi, sioni kwanini tusibanane ili kurejesha nidhamu ya box la kura.
 
Msajili msaidizi wa vyama vya siasa mh Nyahuza amevitaka vyama vya upinzani kuacha mbwembwe na kuzingatia sheria tunapoelekea uchaguzi mkuu.

Nyahuza amesema kuna mgombea urais ametoa vitisho vya kuingiza watu barabarani endapo atafeli kwenye uchaguzi wa Rais, mtu huyo amepungukiwa ustaarabu.

Maendeleo hayana vyama!
Akili ndogo siku zote hazifikirii kamwe! Tundu Lissu alisema "Wakiibiwa kura wataingia barabarani, sio kuwa wakishindwa uchaguzi". Mbona mnapenda kuwawekea watu maneno midomoni? Faki Yuu Meni!
 
ngoja tuone kama kweli ataweza KUMWAGA DAMU kama bendera yao ilivyo
20180913_231505.jpg

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Huyo msajili msaidizi asilete porojo atulie huko huko na atutangazie Mgombea wetu 28 Oct.
 
Msajili msaidizi wa vyama vya siasa mh Nyahuza amevitaka vyama vya upinzani kuacha mbwembwe na kuzingatia sheria tunapoelekea uchaguzi mkuu.

Nyahuza amesema kuna mgombea urais ametoa vitisho vya kuingiza watu barabarani endapo atafeli kwenye uchaguzi wa Rais, mtu huyo amepungukiwa ustaarabu.

Maendeleo hayana vyama!
Nafuatilia hapa live mkutano wa Nccr Mageuzi, kama hizi thread mnazoanzisha hapa JF ndio huwa mnaokoteza maneno mawili matatu ya mtu na kuanzisha thread basi tuna msiba.

Haya sasa Joseph Butiku yupo live anavikemea vyombo vya dola anzisha uzi basi.
 
Back
Top Bottom