Uchaguzi 2020 Msajili wa Vyama ameionya CHADEMA kwa kuongeza ubeti wa 3 katika Wimbo wa Taifa jana katika Mkutano wa Baraza Kuu

Ni kweli wimbo wa taifa huimbwa kwa sauti ya kwanza, ya pili, ya tatu na ya nne, wao sauti hizo zilichanganyika zikawa mazagazaga.
Nkosi zikelele Africa...™
 
Ndugu! tofautisha marumbano ya vyama na utii kwa taifa. Kama wanachezea wimbo wa taifa ambao ni utambulisho wetu sote wakidhani wanashindana na ccm, wanakosea. Hii ni maudhi ya watanzania bila kujali itikadi za kisiasa.

..tatizo ni ccm kujiona wao ndiyo watii zaidi kwa taifa na ndugu zao walioko ktk vyama vingine ni watu baki.

..nimeangalia clip ya walichofanya cdm sijaona kama hawakuuheshimu wimbo wetu wa taifa.

..kama wewe umeudhika basi pole sana, lakini tuko wengine hatuoni kama cdm wamefanya makosa na hatujaudhika hata kidogo.

..Nchi hii ni yetu sote. Tusibaguane. Tusikomoane. Tusitafutiane visa. TUJENGE NCHI PAMOJA.
 
Chadema wamevunja kifungu gani cha sheria??? Huyu ni Jaji tunategemea atoe uthibitisho wa hicho kifungu cha sheria kilichovunjwa
 
Aposema wamevunja sheria, msajili ni vyema angeinukuu sheria na kifungu husika ili jamii iweze kufahamu.
 
Ikiwa kisheria wimbo wa Taifa ni hizo beti mbili basi ukiongezeka ubeti wa tatu huo kisheria siyo wimbo wa Taifa tena ila wimbo tu wa mtaani.

Tatizo ni kama huo wimbo una patent kisheria.
Kumekucha kumekuchaaaa
 
..sheria ya KUNAJISI wimbo wa taifa.

..Msajili anataka kuwatoa CDM kwenye reli.
Magufuli ndiyo anayenajisi kila kitu....Kuku, jogoo nk. Tangu lini ukasikia "KUKU HOYEE" huko si ndiyo kunajisi haki za wanyama...anawa-stress wanyama. Huyo msajili anaona hilo ni sawa tu? Bado anaendelea kunajisi vitu vingine.
 
Weka video acha kubwabwaja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hawawezi kuheshimu wimbo wa Taifa tuwaelewe vipi? Ulishawahi kusikia wapi wimbo wa Taifa unaimbwa tu kiholela?

Haya mambo mbona hata mtoto wa darasa la kwanza anajua wazi kwamba ni kosa na halikubaliki kuedit kwa wimbo wa Taifa?

Hivi hiki chama hakiwezi tu hata kuedit wimbo wa Diamond ni kosa kisheria sembuse wimbo wa Taifa
 
Sisi wananchi tunawaona tuu wanayofanya CDM. Wabishane kwa hoja na sio kubadili mambo yetu ya kitaifa.
Kuna watu wanavaa chupi zenye rangi na mpangilio wa bendera ya taifa.

Kuna watu wanavaa nguo zenye rangi na mpangilio wa bendera ya taifa. Kuna watu wanavaa tai zenye rangi na mpangilio wa bendera ya taifa.

Kuna watu wanatumia vitambaa vyenye rangi na mpangilio wa bendera ya taifa kama vitambaa vya mkononi kupengea kamasi. Hebu tuelezee,hawa hawa hawajabadili mambo yetu ya kitaifa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…