Msajili wa vyama vya Siasa unasubiri nini kuifutia usajili CHADEMA wakati inaendelea kukiuka sheria na kuchochea chuki na ubaguzi?

CHADEMA wanahamasisha na kuchochea ubaguzi kati ya wananchi wa Zanzibar na Bara,wanasema wazanzibari hawana haki huku Bara,wanasema hawastahili kushika uongozi ikiwepo Urais ,wanataka na kudhamiria na kutaka kuhamasisha kuuvunja muungano.
Je mtanganyika wa bara anaruhusiwa kuwa hata balozi wa nyumba kumi huko zanzibar? Tuonyeshe kiongozi mmoja tu huko zanzibar ambaye ni mtanganyika, huu ujinga sijui utawatoka lini.
 
Sijajua kama ni ubaguzi kusema Fulani ni mzanzibar.

Nchi hii ina watanzania na Wazanzibar na Tunakatiba ya Tanzania na ya Zanzibar.

Hivyo kuna watanzania na kuna Wazanzibar kwamujibu wa katiba ya nchi ya Zanzibar. Nl katiba ya Zanzibar Sura ya 1(1) inaeleza kuwa Zanzibar ni moja ya nchi zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ikiwa Zanzibar ni nchi maana yake ina raia wake kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar na raia wake wanaitwa Wazanzibar. Mpaka hapa swali linakuja Je ni katiba ya ZanzIbar yenye ubaguzi au ni raia wa Tanganyika wanapoamua kuifuata na kuitumia kwenye mazungumzo wanakua na ubaguzi.

Nadhani shida ni Aina ya muungano na kero za muungano ambazo utatuzi wake bado mpaka sasa. Tuungane iwe nchi moja yenye serikali moja au serikali tatu ili kusiwe na ubaguzi.

Tatizo linahitaji utatuzi sio watu wakilizungumzia kwa uwazi ionekane ni wabaguzi. Kwanini kuwe na serikali ya Zanzibar ikiwa sisi ni wamoja na hatubaguani?

Ukiuliza mambo ya Tanganyika kwa sasa yasiyo ya muungano yanasimamiwa na Kiongozi gani?? Unaweza kuchanganyikiwa na usijue kabisaa.
 
Jaribu kujielisha kufahamu muundo wa muungano wetu ulivyo na sababu ya kuwa hivyo.
 
Kuwaza kufuta CHADEMA ni upeo mfupi wa kufikiri, huwezi kuwa Greet thinker usijue ukubwa wa kazi zilizofanywa na Chadema kuibua mambo nchi hii, nachelea kusema
'Ushabiki' ni neno sawa na 'uhuni'
Kuchochea ubaguzi ndio kazi kubwa? Kupandikiza chuki ndio kazi kubwa.
 
Luca,lazima una homa ya bonde la ufa/the rift valley fever.Yule mwana CCM aliyediriki kuuambia umma wakiwapoteza wakinzani wasiwatafute ulimchukuliaje?Kwa nini msajili asianze na hicho chama cha aliyetamka hayo?
 
Luca,lazima una homa ya bonde la ufa/the rift valley fever.Yule mwana CCM aliyediriki kuuambia umma wakiwapoteza wakinzani wasiwatafute ulimchukuliaje?Kwa nini msajili asianze na hicho chama cha aliyetamka hayo?
Alishakemewa na kulaaniwa kwa kauli yake. Je ni wapi CHADEMA wamelaani kauli za viongozi wao kutoa maneno ya kibaguzi hadharani?
 
Wewe umepata chuki gani? unapigana na Katiba? Samia hatoki Zanzibar ni uongo? Zanzibar haina Rais wake? Kwanini Arusha, Dodoma au Morogoro haina Rais wake?
Dogo ungetulia tu uache wenye akili timamu ndio wajadili hoja hii maana wewe akili yako haiwezi ikaelewa
 
Dogo ungetulia tu uache wenye akili timamu ndio wajadili hoja hii maana wewe akili yako haiwezi ikaelewa
Amekueleza ukweli. Unamzungumziaje yule mbunge anayewakilisha watu kumi na tatu kutoka Zanzibar aliyesema watu wa Tanganyika wakitaka kwenda Zanzibar wawe na pasipoti?
 
Mama na baba wa hayo ni CCM
Chama changu kimeasisi kila aina ya uovu. Na hata wewe ni sehemu ya disgrace ya nchi.

Kwanini Msajili asikifute?
 
Amekueleza ukweli. Unamzungumziaje yule mbunge anayewakilisha watu kumi na tatu kutoka Zanzibar aliyesema watu wa Tanganyika wakitaka kwenda Zanzibar wawe na pasipoti?
Alishakemewa na kupingwa hoja yake hadharani tofauti na hao nyumbu wa CHADEMA ambao wanaunga mkono ujinga wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…