Nukuu Ya kitabu Hicho Ukurasa wa 3..
"
Tanzania ni lulu ya pekee kabisa katika historia ya Afrika huru. Nchi nyingine zote ni za kurithi kutoka kwa wakoloni. Wako watanzania wa ajabu kabisa wanaosema kuwa uamuzi huo, au vyombo vilivyotumiwa au njia iliyotumiwa, au vyote, navikuwa halali. Hao hawana shaka na uhalali wa Tanganyika ambayo iliunganishwa na Wajerumani, na ikamegwa megwa na Waingereza na wenzao. Kwa hao, kama Rwanda na Burundi na Tanganyika zisingetengwa na mabeberu, tukazirithi kama zilivyokuwa chini ya Wajerumani, wasingeushuku uhalali wa nchi moja hiyo. Lakini kama baada ya uhuru, Rwanda na Burundi na Tanganyika zingeamua kuungana ziwe nchi moja, kwa utaratibu wowote ambao zingekubaliana, 'wazalendo' hawa wangesema muungano huo sio halali."
Kitabu Hicho Hakiobyeshi Kwanini Tanzania Iliimeza Tanganyika na Kuacha Zanzibar ikiwa Bado iko Huru..
Nimekisoma kitabu, Nakisoma kitabu na Bado nitaendelea kukisoma Nahisi Nimeanza kukisoma kabla hujazaliwa Lucas..
Kitabu Hicho Kinaeleza Falsafa za Mwalimu nyerere Kuhusu Muungano na Kutoencourage Utengano au Kuvunja Muungano..
Ila hakielezi kwanini Tanganyika Ilikufa wakati zanzibar ikibaki na huo ndio msingi wa Hoja Yangu..
Na hata Fatume karume Kama Ulimsikiliza Alisema Kuwa hio ni Mindset mbaya Kuliko zote.. Hakuna Mtu hakubali Muungano Ila Muungano.wa Kufunika Nchi moja na kuacha nchi nyingine hatuufurahii..
Tafuta Journal ya CIA Inaitwa Tanzania "States within a state ya mwaka 1977 kama sikosei"
View attachment 2977506