Msajili wa vyama vya Siasa unasubiri nini kuifutia usajili CHADEMA wakati inaendelea kukiuka sheria na kuchochea chuki na ubaguzi?

Msajili wa vyama vya Siasa unasubiri nini kuifutia usajili CHADEMA wakati inaendelea kukiuka sheria na kuchochea chuki na ubaguzi?

Majibu yalitolewa ndani ya bunge ambamo kauli ilitolewa.
Lucas Mimi Nina Amini kabisa UVCCM wengi ni wasomi Pengine kushinda hata Hao BAVICHA..

Na naamini kwa kuwa Nimelea UVCCM wengi na wamepita mikononi mwangu..
Kwakuwa Wewe ni UVCCM..

NA mimi nimekuomba Unionyeshe Makosa Ya Lisuu Kisheria sio Kiutashi, Maana Kiutashi kweli anajaribu Kubagua watu na Kuzua Taharuki ila Kisheria Hana Kosa
 
Kasome sheria ya vyama vya siasa juu ya makatazo kwa vyama vya siasa. Kasome 6:0
 
Siwezi kunyamaza napoona CHADEMA kwa uroho na uchu wake wa madaraka inaeta kauli za kuchochea ubaguzi na machafuko hapa nchini pamoja na kuvunja muungano wetu huu adhimu.
Muungano Wetu Uko hivii.
A+B= C+B
Tanganyika + Zanzibar = Tanzania + Zanzibar..

Watu wanachohoji!

Hata kama Zanzibar Ina umri Mkubwa kuliko Tanganyika ila Lilippkuja swala la Muungano kwa nini Tusingeungana na Kuunda Nchi Moja na sio Nchi moja kufutika na nyingine kubaki..

Leo hakuna Nchi ya Tanganyika Ila kuna Nchi ya Zanzibar..
 
Kasome sheria ya vyama vya siasa juu ya makatazo kwa vyama vya siasa. Kasome 6:0
Habari Tena Lucas..

Hii haitiwi Sheria ya Vyama vya Siasa..
Uliyoandika Inaitwa Kanuni ya Vyama vya Siasa Itokanayo na sheria ya vyama vya Siasa..
Na inasema Kipindi cha Uchaguzi maana yake kwenye Kampeni za Uchaguzi kwa bahati mbays Lissu hakusema Hayo kwenye Kipindi cha Uchaguzi

Na hiyo uliyotaja Ni kanuni namba Sita..
Screenshot_20240430_143344_Adobe Acrobat.jpg

Kwa Mujibu wa Lissu Kumuita Mama samia Mzanzibar hajapingana na Katiba ya Tanzania wala katiba ya Zanzibar...

Kumuita Mama Samia Mzanzibari haipingani na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ibara ya 6 na ibara ya 7
Screenshot_20240430_143919_Adobe Acrobat.jpg
 
Muungano Wetu Uko hivii.
A+B= C+B
Tanganyika + Zanzibar = Tanzania + Zanzibar..

Watu wanachohoji!

Hata kama Zanzibar Ina umri Mkubwa kuliko Tanganyika ila Lilippkuja swala la Muungano kwa nini Tusingeungana na Kuunda Nchi Moja na sio Nchi moja kufutika na nyingine kubaki..

Leo hakuna Nchi ya Tanganyika Ila kuna Nchi ya Zanzibar..
Unachokitaka hicho cha kwanini tusingekuwa na serikali moja nimekwambia usome kitabu cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania ,kilichoandikwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Na wewe ukasema umekisoma. Ila nimegundua hujakisoma na kama ulikisoma basi umesoma jina la kitabu tu kwa nje .na kama ulisoma chote basi hukukielewa hata kidogo na ulikisoma akili ikiwa haijatulia. Maana kama ungekisoma kwa kutulia kwa hakika usingeuliza maswali hayo uliyouliza ambayo majibu yake kwenye kitabu hicho.
 
Nukuu Ya kitabu Hicho Ukurasa wa 3..

"Tanzania ni lulu ya pekee kabisa katika historia ya Afrika huru. Nchi nyingine zote ni za kurithi kutoka kwa wakoloni. Wako watanzania wa ajabu kabisa wanaosema kuwa uamuzi huo, au vyombo vilivyotumiwa au njia iliyotumiwa, au vyote, navikuwa halali. Hao hawana shaka na uhalali wa Tanganyika ambayo iliunganishwa na Wajerumani, na ikamegwa megwa na Waingereza na wenzao. Kwa hao, kama Rwanda na Burundi na Tanganyika zisingetengwa na mabeberu, tukazirithi kama zilivyokuwa chini ya Wajerumani, wasingeushuku uhalali wa nchi moja hiyo. Lakini kama baada ya uhuru, Rwanda na Burundi na Tanganyika zingeamua kuungana ziwe nchi moja, kwa utaratibu wowote ambao zingekubaliana, 'wazalendo' hawa wangesema muungano huo sio halali."

Kitabu Hicho Hakiobyeshi Kwanini Tanzania Iliimeza Tanganyika na Kuacha Zanzibar ikiwa Bado iko Huru..

Nimekisoma kitabu, Nakisoma kitabu na Bado nitaendelea kukisoma Nahisi Nimeanza kukisoma kabla hujazaliwa Lucas..

Kitabu Hicho Kinaeleza Falsafa za Mwalimu nyerere Kuhusu Muungano na Kutoencourage Utengano au Kuvunja Muungano..

Ila hakielezi kwanini Tanganyika Ilikufa wakati zanzibar ikibaki na huo ndio msingi wa Hoja Yangu..

Na hata Fatume karume Kama Ulimsikiliza Alisema Kuwa hio ni Mindset mbaya Kuliko zote.. Hakuna Mtu hakubali Muungano Ila Muungano.wa Kufunika Nchi moja na kuacha nchi nyingine hatuufurahii..

Tafuta Journal ya CIA Inaitwa Tanzania "States within a state ya mwaka 1977 kama sikosei"
20240430_151001.jpg
 
View attachment 2977506
Soma eneo ambapo mwalimu Nyerere anazungumzia sababu ya kutoungaisha nchi zetu na kuwa nchi moja.na sababu ya kuiachia Zanzibar mamlaka ya kubakia kama ilivyo sasa.
 
Soma eneo ambapo mwalimu Nyerere anazungumzia sababu ya kutoungaisha nchi zetu na kuwa nchi moja.na sababu ya kuiachia Zanzibar mamlaka ya kubakia kama ilivyo sasa.
Muungano ni mzuri, lakini Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume walikosea kutukuondoa utambulisho wa Mzanzibari. Makosa hayo ndio yamesababisha muungano kuonekana wa upande mmoja, na iliyokuwa Tanganyika kuonekana ni " shamba la bibi " la Wazanzibar kufanya wanavyotaka.
 
Soma eneo ambapo mwalimu Nyerere anazungumzia sababu ya kutoungaisha nchi zetu na kuwa nchi moja.na sababu ya kuiachia Zanzibar mamlaka ya kubakia kama ilivyo sasa.
Lucas!

Eneo Hilo ulilotaja ni Ukurasa wa 18 Wa kitabu hicho na Wazo hilo Halijengi Hoja na Huwezi kuita Sababu ya Kudiverge Kwenye Mifumo Sahihi ya Muungano Na Kwenda kwenye Mfumo Ambao si wa Kimuungano kwa Kuwa tu unaogopa watu watakuonaje ukifanya Hivyo..

Katika Ukurasa huo Nyerere anataja Aina za Serkali za Muungano anasema Serikali za Muungano ziko Aina mbili..

  • Serkali ya Muungano wa Shirikisho la serkali tatu (Kama ilivyotaja Katiba ya Waryoba) Yaani Tanganyika,Zanzibar na Serikali ya Muungano wa Tanzania
  • Serkali Moja yaani Tanzania Bila kuwepo kwa Serkali ya SMZ
Akasema serikali Tatu haiwezekani kwa Kuwa Kipindi hicho Tanzani haikuwa na Pesa za kutosha..
kwa pendekezo likawa ni serkali Moja..

Hata hivyo akashindwa kwa kuwa Aliogopa Mafikirio ya watu wa magharibi kwamba ataonekana anaitawala Zanzibar..

Screenshot_20240430_160933_Chrome.jpg

Sasa Maelezo haya yote Ya nyerere Bado hayajibu Hoja kwanini Aliamua Kuiacha Serikali ya Zanzibar kwa sababu Vipi pale Tanzania Ilipopata pesa Kwanini wasingeendelea na wazo la kwanza la Serkali tatu??

Kingine wazo la mtizamo wa Nchi za Kimagharibu lilikuwa wazo la kidhaifu sana Na ndo maana nasema mpaka sasa Bado hatuna sababu kwanini..

Na ndo maana Nikakuambia soma ile Doccument ya CIA ya mwaka 1977 Wakati huo maandishi ya nyerere yalichapwa mara ya kwanza Mwaka 1993 Baada ya Kikao cha Kamati kuu cha CCM..

20240430_151001.jpg
 
Ni lazima tupinge kwa nguvu zote na kukemea chuki na ubaguzi unaotaka kupandikizwa na CHADEMA kwenye Taifa letu.
Katoa ufafanuzi.....kasome katiba ya Zanzibar........halafu ndio utoe hukumu. Yule Mbunge wa Zanzibar aliotaka watanzania kutoka bara waingie Zanzibar kwa Passport, sio mbaguzi.?
 
P
CHADEMA wanahamasisha na kuchochea ubaguzi kati ya wananchi wa Zanzibar na Bara,wanasema wazanzibari hawana haki huku Bara,wanasema hawastahili kushika uongozi ikiwepo Urais ,wanataka na kudhamiria na kutaka kuhamasisha kuuvunja muungano.
Umbavu kabisa wewe. Ulishawahi kuishi visiwani lakini ukajionea watu wa bara wanqvyobaguliwa au unakata mauno yu hapo lumumba? Ivi unajua maana ya kuhamasisha vurugu wewe??
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nauliza kwa uchungu mkubwa sana kuwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ipo wapi? Inafanya kazi gani? Imelala wapi huko usingizi wa pono mpaka inashindwa kuona hatari kubwa inayoletwa na CHADEMA hapa nchini? Msajili unaendeleaje kupokea mshahara ambao ni kodi zetu watanzania wakati unatuweka hatarini watanzania na amani ya Taifa letu?

Sheria ya vyama vya siasa inakataza na kupiga marufuku kabisa kwa chama chochote cha siasa kufanya siasa zenye kuchochea ubaguzi kwa misingi ya Udini, ukabila na hata ukanda.sheria inakataza pia kwa chama cha siasa kunadi sera zinazohamasisha au zenye lengo la kuvunja muungano wetu au zenye lengo za kufanya siasa za upande mmoja tu wa muungano.

Lakini leo hii tunashuhudia CHADEMA kupitia viongozi wake wakichochea chuki kali sana na kupandikiza uasi wa kuuvunja muungano wetu pamoja na kuchochea ukanda pasipo kuchukuliwa hatua za aina yoyote ile.ni hatari sana hii inayokuja kwa Taifa letu ikiwa hali hii ya kupandikiza mbegu za ubaguzi itaachwa iendelee kuhubiliwa na kuenezwa na CHADEMA.hii siyo siasa tuliyoitaka watanzania.hatukutaka siasa za kuja kutugawa watanzania na kulipasua Taifa letu.

Tulihitaji siasa za hoja,siasa za sera mbadala, siasa za fikira na mawazo mbadala juu ya ujenzi wa Taifa letu,siasa za hoja ya namna bora ya kulipeleka mbele Taifa letu .Siasa za mawazo mapya ya namna bora ya kutumia rasilimali zetu kwa usahihi katika kuinua uchumi wa Taifa letu na kuboresha maisha ya watanzania wote pamoja na usambazaji wa huduma za kijamii pamoja na kupunguza utegemezi.

Lakini inaogopesha na kutisha sana tunapoona CHADEMA imebadili majukwaa ya kisiasa kuwa uwanja wa kuwasha moto wa kuchochea machafuko kwa Taifa letu.chadema wameishiwa hoja za kuwashawishi watanzania na sasa wameamua waanze kupandikiza mbegu za ubaguzi na chuki kwenye mioyo ya watanzania. Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana ,ni sawa na kula nyama ya mtu ambapo huwezi ukaacha ukishakula nyama hiyo.

leo CHADEMA wameanza kupandikiza mbegu ya ubaguzi ,jinsia , ukanda na mengine mengi.hawataishia hapo bali wataenda mbele zaidi kuanza ubaguzi wa mkoa na mkoa kwa kusema mkoa huu unachangia mapato makubwa sana na hivyo ujitenge na kupewa hadhi ya aina yake.

Msajili wa vyama vya siasa amka ofisini haraka sana uchukue hatua kali sana kabla nchi haijaingia katika matatizo ambayo yatalisambaratisha na kuligawa Taifa vipande vipande. Tumia sheria kuwaadhibu CHADEMA kwa kuwa tayari wameshavunja sheria zote za usajili wao .na sasa wanastahili kufutiwa usajili. Mambo yanaanzaga hivi hivi mpaka mwisho inakuwa donda ndugu litakalolitesa Taifa lote..

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa,.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Kama wanaweza Magufuli angeweza. Msijidanganye hamna uwezo wa kufuta vyama vya wananchi. Vyama sio mtu ni watu. Msidanganye watu kwamba mna uwezo wa kufuta chama cha wanachama 10M
 
P

Umbavu kabisa wewe. Ulishawahi kuishi visiwani lakini ukajionea watu wa bara wanqvyobaguliwa au unakata mauno yu hapo lumumba? Ivi unajua maana ya kuhamasisha vurugu wewe??
Mwenye akili anajibu hoja kwa hoja na siyo matusi.ila kwa kuwa wewe huna akili ndio maana umetumia matusi kuonesha ujinga wako uliokujaa kichwani mwako.
 
Kama wanaweza Magufuli angeweza. Msijidanganye hamna uwezo wa kufuta vyama vya wananchi. Vyama sio mtu ni watu. Msidanganye watu kwamba mna uwezo wa kufuta chama cha wanachama 10M
Hao watu millioni kumi uliwatoa wapi? Acheni kuwa wajinga jinga tu.
 
Utavunjika wewe na kuiacha Tanzania ikiwa moja na imara zaidi.
Ingekuwa muungano ni imara usingeanzisha uzi wa kulia lia kwa saab ya speech moja ya Babati...

Leo hii ukisimama jukwaani Marekani kuukandya muungano wao hakuna atakaekujibu, hakuna atakaekosa usingizi, hakuna atakaekutisha. Mjadala wa Muungano wao ulishakwisha.

Speech ya Babati ya Tundu Lissu imeshtua dola, imeamsha Watanganyika, inajadiliwa bungeni, inajadiliwa vijiweni, inajadiliwa mitandaoni ... Ametikisa Muungano...

Huwezi kubisha, he shook the weak arse Muungano!
 
Ni vyema ungesubiri mada za kulingana na akili yako hiyo ndogo.maana mada hii ipo juu ya uwezo wako.
Punguani, ni lini uliwahi kuleta mada ya maana JF, zaidi ya hizi kilele za kipuuzi?

Mwombe msajili akufute wewe usiye na lolote la maana kwa nchi. Kodi hulipi, mawazo ya maana huna. Umebakia tu na uchawa ili urushiwe makombo kama yule anayebweka.
 
CHADEMA ni lazima wakemewe kwa nguvu zote kwa hili wanalotaka kulileta hapa nchini baada ya kuwa wameishiwa hoja za kuwashawishi watanzania kuwaunga mkono.
Jibu hoja za lisu acha kulialia hapa. Kwani huo muungano ni msahafu wa dini usijadiliwe? Itisheni kura ya maoni mpate maoni ya wat juu ya huo muungano wa kibaguzi
 
Back
Top Bottom