Msamaha kubutuliwa, Ndugai aungwe mkono


Pamoja na yote imeandikwa - dhambi hata kama ni nyekundu kama bendera zitakuwa nyeupe kama theluji.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kuomba msamaha bila kujua kosa lake ndio kosa alilofanya Ndugai, mwenyewe anasema alitoa maoni yake kwa nia njema, matokeo yake kumuomba kwake msamaha mjinga ndio malipo yake ameyavuna leo.

Mjinga siku zote huwa haombwi msamaha, kwani kwa kufanya hivyo atazidi kuwa mjinga kwa kuamini ujinga wake ni maarifa, na atazidi kuwadharau waliomzidi maarifa matokeo yake atazidi kuwatumbukiza shimoni anaowaongoza kwa ujinga wake.

Naungana nawe mleta mada kwenye kutumia issues zinazoleta mpasuko upande wa pili zenye tija kwa jamii, kujidai special tunaoweza kujifanyia kila kitu peke yetu ni kuzidi kujichimbia kaburi letu, let brave mind play some tricky games, hakuna siasa isiyounganisha hitaji la makundi tofauti.
 

Hizo ajenda zote wapinzani tunaweza kuzisimamia bila kutegemea mshikamano wowote na hao wachumia tumbo. Hatuko tayari kuungana na wahuni, kisa ajenda zetu kwa bahati mbaya na wao wameziangukia. Hao wahuni wapambane na hali zao, lakini sisi sio wa kuwapa ahueni kwenye vita yao ya madaraka.
 
Chadema watakuwa wajinga wakirudia makosa waliyofanya kwa Lowassa, Sumaye na Nyalandu.
 
vyovyote iwavyo, kukopa trillion 10 ndani ya miezi 9 kwa ajili ya madawati hatuwezi kukubali, hili lazima liondoke na mtu!
Poleni sana, leo ndio ameamua kuwapa za uso sukuma gang!!hayo mamiradi lukuki yaliyoanzishwa kwa kukurupuka pesa zake za kuyaendeleza ujenzi zinatoka wapi?eti trilioni 10 kwa madawati!!huyo shujaa wenu aliyekuwa anasema hakopi , ila daa mungu fundi sana, kwani ametuepushia mengi!!
Leo sasa ndio ametangaza vita ni vita mula, kama mlimtuma Ndugai ujumbe mmeupata.
 
Mwacheni kila mtu apambane na hali yake mwenyewe.
 
Kwa kauli zile za Mama, hata huo msamaha wa JN inaonekana amefanya kwa shinikizo baada ya kutonywa kwa yajayo. Lazima kuna mtu kavujisha siri ili amuokoe Mzee wa Galilaya. Wakaona kuomba radhi hadharani inaweza kunusuru.
Ila Mama anaenda kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na ndiyo utakuwa mwisho wake na wanaweza kumshitaki akafungwa.
 

Chimbuko la kufikia kuomba msamaha yawezekana kuwa kaingizwa chaka, pengine na washirika wake hasa hasa baada ya kuendelea kuzodolewa na kukosa waungaji mkono wa hadharani.

Kama uzi huu unavyolenga kwa hakika "lose ball" hii ilipaswa kuchukuliwa kimkakati tangia ilipoanza kuzagaa zagaa bila mwenyewe kwenye lango la adui.

Kwa hakika tunapaswa kutambua ushindi ni magoli na adui si wa kudumu, ila agenda.

Tupigane "total football" na aina zote za silaha akili vichwani.
 
Chadema watakuwa wajinga wakirudia makosa waliyofanya kwa Lowassa, Sumaye na Nyalandu.

Makosa yapi yaliyofanywa kwa hao. Walikuja wakafanya sehemu yao. Walipoona nyimbo za sayuni haziimbiki wakaondoka. Shida iko wapi?

Slaa alipoona hakuimbiki aliondoka kama domokaya wa kule nanihii tu.

Hakuna rafiki wala adui wa kudumu. Ni lazima ku perfect kwenye hilo.
 

Siasa ni science mjomba. Siasa ni mikakati ikibidi hata infiltration kwa adui ni sehemu ya mchezo.

Hatuna ya kujifunza hata Kenya tu?

Bila kuufahamu mchezo huu kikamilifu, matokeo ya kupata wiki ijayo tunaweza yapata baada ya miaka 10.

Kwani ujinga utakuwa ni nini basi?
 
Ila Mama anaenda kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na ndiyo utakuwa mwisho wake na wanaweza kumshitaki akafungwa.
Hahaaaa!!!hilo haliwezekani kamwe kwa siasa za kiafrika!!kwanza kwa michambo hiyo wote walio nyuma ya Ndugai wamesha kula kona!!na leo sasa ndio ametangaza kiama baina yake na sukuma gang!!ila Mungu anatisha kweli Ndugai wa mwaka mmoja tu uliopita alivyokuwa anawafanyia wenzake leo ni ya kumkuta haya?!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…