Mbona inajulikana kwa nini wachaga waliona kama wanaonewa lakini ni ukweli usiopingika kuwa wachaga walikuwa wanafaidika sana na ufisadi wa siku za nyuma ndiyo maana walipoanza kushughulikiwa waliona kama wanalengwa wao wakati walikuwa wanalengwa mafisadi na si ukabila.
Jameni, hivi mbona hatuelewani kwa jambo rahisi namna hii?
Kuna waTanzania wangapi wenye asili ya waChaga hapa nchini?
Ni ushahidi gani ulionao wewe unaoonyesha kwamba watu wote hao "walikuwa wanafaidika na ufisadi wa siku za nyuma..."; ushahidi wa hili kweli unao wewe?
Kwa nini uhusishe matendo ya watu wachache ndicho kiwe kielelezo cha jumuia nzima; kwa nini?
Huko uchagani hakuna wasiokuwa na chochote, kama walivyo waTanzania wengine toka sehemu mbalimbali hapa nchini?
Kwa nini hawa nao uwalaumu, kwa makosa ambayo hawayajui kabisa?
Kwa nini sheria zisiwashughulikie hawa wachache wanaofanya ufisadi bila kujali asili zao ni zipi?
Nini hasa faida inayotokana na kutuweka waTanzania kwenye makundi ya namna hii?
Huoni kwamba nyinyi ndio mnaozidi kuchochea moto wa ufarakano ndani ya taifa hili?
Ninatambua sana msimamo wako unaoambatana na jina lako "magu2016" na aina ya michango unayoweka humu; lakini kuna nyakati inabidi binaadam ujipime kama unayofanya yana manufaa kwenye jamii unayoipigania au yanaongeza tu uchungu na mifarakanyo.
Kwa nini tuzidi kuchochea mifarakanyo, si bora kunyamaza tu!