Kwanza kabisa Kwa CCM navyoijua, wao watayachukua haya maneno 2025 na kuwaambia wasukuma kwenye campeni zake kuwa, tulipompa nchi mwenzetu msukuma jembe, tingatinga, wakaanza kuwaita Sukuma gang, mtawapaje Kura hawa wapinzani wabaguzi??
Jina hili la Sukuma gang, najua hata wa CCM Baadhi wanalitumia, lakini 2025 litakuwa mtaji wao, na kiukweli wapinzani wanaweza kupata tabu Sana,
Mimi ni mchaga, lkn kiukweli hili jina Sukuma gang, naliogopa linaweza kuleta shida badaye, na likiendelea, Mungu akituweka hai, nitakuwa wa Kwanza kuwauliza maswali wapinzani kwenye Kampeni zao huko mikoa ya ziwa kuhusu jina hili la kichochezi,hivi Kwa mfano, msukuma atampaje Kura mpinzani ili Hali mpinzani hataki Kumuona msukuma Mbele yake?