Msikilize vizuri mtaalamu wao wa IT. Na kwa uzoefu wangu mtaalam wao wa IT yuko sahihi. Hapa yawezekana kuna conspiracy.
Kwa kawaida kuna admin account yenye login details ambazo ufichwa na institution. Halafu admin wa database anaitumia hizo login details kufungua admin account yenye mamlaka ya juu kama ile itakayotunzwa na ofisi. Kutumia account ya marehemu ni rahisi sana, kwa sababu kwa kutumia ile akaunti ya juu, password ya marehemu inabadilishwa na mtu mwingine ku-access database kwa jina la marehemu. Haitaji kuondoa jina au akaunti ya marehemu ili kufanya uhuni kwenye database, kwa sababu yawezekana iliondolewa halafu ikatengenezwa tena ila itaonesha tarehe ya kufunguliwa.
Halafu kama kuna parameters ambazo zilisetiwa kabla ya uchaguzi na hazikutakiwa kubadilishwa tena, zimebadilishwa basi tume lazima itoe maelezo.