TANZIA Msanii Albert Mangwea afariki dunia

TANZIA Msanii Albert Mangwea afariki dunia

Mods wanabishana nini.?
Mbona hii theard inayumbishwa sana.?

Huyu ni msanii mkubwa Tanzania hata kama alikua na sifa mbaya anastahili heshima kwa alioufanyia mziki wa Tanzania.!!
 
Marehemu alizidisha dozi ya kujidunga
 
Kama ni sembe asepe tu.

Mkuu rudia mara mbili ulichoandika, yaweza mkuta ndugu yako, wewe mwenyewe au hata rafiki yako wa karibu, jiulize je ww utapenda watu waseme maneno hayo uliyoandika?
 
Na nyie mods mbona mna kiherehere hivyo? Ndo nini sasa kuihamisha hamisha hii mada...mara muipeleke selebrite mara muilete habari mchanganyiko mara muirudeishe tena selebrite....mmelewa gongo nyie?
Itakua wanabishana huko.!!
 
#FAHAMU sammisago @nikkwapili noma, kuna watu wanne wamenipigia,wanassema wapo SA
wananipa stry tofauti kabisa 8:36 p.m. Tue, May 28

Kipi sahihi, kafariki au ni taarifa zisizo sahihi?
 
Last edited by a moderator:
dark master itamgusa sana. mi nahisi itakua sembe ndo chanzo. mchiz mox, noorah, rasta, white na member wote chember squad pole sana. r.i.p. aka. kaObama, mimi. kikwete aliona amsaidie Ray C peke yake wengine akawaacha wateseke hadi kufa. huu ni ubaguzi. mia
 
"vipi DJ haupigi hewani na unasikiliza ghetto na hizi vocal demu wako anapigia nye.to,Q ebu zima instrumental ili machizi wasiwe mamento"-Ngwair
 
Ngwea-22.jpg



MSANII maarufu wa Bongo Fleva, Albert Mangwea maarufu kama Ngwair, amefariki dunia leo akiwa nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa za Redio mbalimbali jioni hii nchini, inadaiwa Ngwair amefariki dunia kutokana na matatizo ya matumizi ya dawa za kulevya.

Kimuziki, Ngwair aliibukia kwenye Dodoma ambako alikuwa katika kundi moja na Noorah na Mez B.
Baadaye akapata dili Bongo Records chini ya mmiliki wa studio hizo, Petter Matthysse ‘P Funk' aliyemuinua zaidi kimuziki na kumfanya awe miongoni mwa wanamuziki nyota nchini.

Wimbo wake wa kwanza kutamba ni Gheto Langu mwaka 2003 ambao ulimpatia umaarufu kabla ya kutoa albamu yake ya kwanza a.k.a Mimi mwaka 2003 ambayo ilimpatia mafanikio makubwa na kubadili maisha yake.

Hata hivyo, mafanikio hayo yalimlevya na kujitumbukiza kwenye utumiaji wa dawa za kulevya, hivyo kujikuta akishindwa kufanya kazi ya muziki kwa usanifu na kuanza taratibu kufilisika hadi kuuza mali zake zote, ikiwemo gari aina ya Jeep.

Ngwair kutoka kwenye kupanga nyumba nzima maeneo ya Sinza, Dar es Salaam akajikuta anarejea kuishi katika ‘magheto' ya washkaji zake sehemu mbalimbali Dar es Salaam.

Mwaka 2010, Athumani Tippo, mmiliki wa maduka ya Zizzou Fashions alijaribu kumuinua tena msanii huyo baada ya kumchukua kwenye lebo yake na kumuwezesha kutoa albamu ya pili, Nge.

Hata hivyo, Nge haikufanya vizuri sana na kuzidi kumchanganya msanii huyo hivyo kutopea kwenye dimbwi la utumiaji wa dawa za kulevya na ‘kuharibika zaidi'.

Mafanikio yake zaidi ni kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005.
Mwaka 2003, msanii Wayne Wonder aliyekuja kutumbuiza kwenye Fiesta aliondoka na CD ya wimbo Mikasi ya Ngwair baada ya kuvutiwa na kibao hicho alichowashirikisha Mchizi Mox na Ferooz. Pumzika kwa amani.

Mbele yako, nyuma yetu Ngwair. RIP.



====

KELVIN GASPER

Redio Clouds:
http://soundcloud.com/cloudsfm-superbrand/ngwair-msiba


Source:
http://bongostaz.blogspot.com/

http://issamichuzi.blogspot.com/2013/05/breaking-nyuzzzz-msanii-wa-bongo.html
.
 
Naona hata TBC wanathibitisha...kifo kikifika ndio kimefika!
 
unajua kama ni kweli poda imelekea kifo chake itakua hawa wasanii wetu hawana ushirikiano maana ni muda mrefu inasemekana uyu jamaa anabwia poda... kwa nini hawa kumsaidia kama ray c??
 
Back
Top Bottom