Msanii Ali Kiba avaa nguo za kike stejini, wanaume wakware wampigia miluzi

Msanii Ali Kiba avaa nguo za kike stejini, wanaume wakware wampigia miluzi

Hakuna vazi la kike wala la kiume haya yote ni kuiga uzungu tu, hivi kibwebwe kile cha nyasi kilikuwa kuna cha kike na kiume?! Ndio maana Tz hatuna vazi la taifa maana miluzi mingi hata ma designer hawawezi kuleta vazi likakosa kelele. Kiba anazidi kung'ara watu wasiopenda maendeleo yake wanatoka povu tu.
 
Kwenye mavazi ni kweli kavaa uhusika, ts not a big deal... tatzo lipo kwenye hayo mapozi ya kike ndipo panaponipa wasi wasi, au na yenyewe ni kuvaa uhusika???
Hata wale mchele mchele wa kwenye mitindo huwa wanatembea kiume!!
 
Ali Kiba ni mwanamuziki,na muziki ni burudani.
Sioni ubaya wowote maana yuko stejini ambako ndiko ofisini kwake.
Binafsi nimeipenda sana,big up Ali Kiba.

Wengine hapa wanatokwa mapovu,wanatoa kejeli kwa Kiba ambaye kwa show moja anaingiza zaidi ya
huku wao walio ofisini (white collar job) wanalipwa laki 3 wanajiona bora!
Huu ni zaidi ya uwendawazimu!

Millioni 15 show ya kiba? wapi na lini? on the otherhand wanawake huwa wanatetea sana watu wenye mienendo kama hii, haya mambo yapingwe vikali ben paul alivaa sketi kama haitoshi akarekodi video anacheza na boxer sasa hivi anaonyesha makalio kesho sijui itakuaje walahi.
 
hawa wanamuziki wetu wakishaanza kwenda ughaibuni tu wasiwasi unaanza kunishika
 
Watanzania wa kawaida...nasikia sana huu msemo Bungeni
 
It is a Lip Sync Battle. . Sio shabiki wa Alikiba ila he nailed it
 
Hii ilikua Lip Sync Battle Mtv Africa kati ya Alli Kiba(Tz) na ndege mnana Simi(Nigeria) simply Alli Kiba akachagua kuimba ngoma ya The late Brenda Fassie(Vulindela kama nimeandika sahihi) ivyo ilabidi avae uhusika kwa kuonekana kama Brenda na mwisho wa battle dogo Alli akaibuka mshindi kama inavyoonekana kwenye picha.
Kama mzee wa wangu marehemu Tx Moshi Williamu alipokua anaimba "Mume wangu kwa nini umeniacha" wakati yeye sio mwanamke ila lengo hadhira imapate ila ladha halisi ya sanaa yake ila kwa kua siku hizi kila kitu kinaangalia kwa kigezo cha timu sishangai watu wakicharurana umu ili kuridhisha nafsi na chuki za upande mmoja nakumbuka hata Joti alishambuliwa kwa kuigiza dada Kiboga ivyo ndivyo tulivyo tabaka la chini tuna furaha kuwananga wenzetu hata kama tunajua Joti sio shoga ila maumivu ya mafanikio yanatulazimisha tumseme tu ili tupate nafuu ya maumivu yetu BTW ni mtazamo wangu tu wa kawaida kwenye hili kama unapenda huu muziki wa sasa jaribu kuangalia behind the scene za video za hawa wasanii kuna vitu vingi utaviona.
Kwa maelezo yako haya, wakiendelea wengine watakua mataahira
 
Dave Chappelle alisema mwanaume wa kiafrika ukianza kuvalishwa nguo za kike ujue kuna agenda ya kupromote ushoga ambao bado haukubaliki katika jamii zetu.
 
DALILI ZA USHOGA MAMBO MENGINE SIYO YA KUFURAHIA KUBAKI AKIWA NA DADAKE HAELEWEKI WAKIKE YUPI WAKIUME YUPI.
 
Back
Top Bottom