Msanii AY azidi kuonyesha mafanikio yake

Nukta5

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2014
Posts
1,182
Reaction score
1,288
Msanii wa Kimataifa Ambwene Yesaya (AY) anayefanya kazi zake za kisanii nchini Tanzania na pia anatamba na wimbo wake mpya unaoitwa ZIGO amezidi kuonyesha mafanikio yake ya kimuziki na kibiashara yanavyomlipa baada ya kutinga na Range Rover yake kwenye msiba wa baba yake Dully Sykes mzee Ebby Sykes. Licha ya kumiliki Range Rover pia AY anamiliki kipindi cha mikasi na duka la nguo lililopo sinza madukani na pia AY mwaka juzi alisema anataka kufungua biashara jijjini Nairobi nchini Kenya.
 

Attachments

  • IMG_0481.jpg
    124.2 KB · Views: 6,359
  • IMG_0489.jpg
    74.4 KB · Views: 5,667
Hata angetembea kwenye bahari mngesema anatembea kisa hajui kuogelea.
 
the baby to the son, the son to the younger, the younger to the MAN..!
 
Hakuna ajabu ay kuja na gari kama hiyo coz ni msanii wa siku nyingi na ana biashara nyingi tofaut na usanii maduka studio mbona kawaida sana na hii ni yake na aliinunua ye kama yeye
 
Hapa ndo napowafaidi wachawi wa bongo.

Mkuu Deo Corleone umenikumbusha uzi wa Mike mushi alipokuwa kwenye mkasi kuna jamaa alianza kumponda sasa yalizuka mabishano makali sana bila shaka yalizimwa na moderator maana jamaa baada ya kumponda alituhumiwa kuwa ni mchawi na jamaa aliahidi kuleta ushahidi kuthibitisha kuwa kuwa jamaa aliye kuwa anaponda ni mchawi na ni mshirikina na hakika watu wengi walisubiri hule ushahidi! kwakweli nilicheka sana siku hile!

Pia umenikumbusha kuna jamaa alikuja na uzi siku moja akisema watanzania wengi ni wachawi! Kwakweli hizi nyuzi zilinichekesha sana na nilijifunza kitu kutokana na nyuzi hizo!
 
Last edited by a moderator:
Hazina issue hizo hata 35m unapata,weka ghorofa lake tulione.

Jana limeona gari kama hilo pale opossite na millenium tower likiwa linauzwa 49milion. Atakayepata muda kesho apite lipo kandokando ya barabara na bei ipo kwenye kioo cha mbele.

Ni kweli hayo magari sio issue...kama vp tuonyesheni ghorofa lake tumpe heshima.
 
Hata angekuwa na Bentley ,bado ungetaka Lamborghini!!

Muacheni na maisha yake.

Sidhani kama umewahi hata kumchangia hata jero


Kuna kijana kamchomea mwenzie vyeti vya shule kuhojiwa sababu anasema roho inamuuma mwenzie akienda kazini ilhali yeye anazagaa tu mtaani life lake gumu...

Waafrika tumeumbwa kiunyama Sana wivu unawafanya watu kuwa wachawi.
 
Kuna watu Jf kazi yao kukashfu tu acheni ujinga kama si lake we unalo ni mafanikio yake ila upumbavu umewajaa watu wengi humu Jf shenzi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…