Msanii Bando MC hajui 'Ku-Rap'

Si kila mtu anataka kufanya unavyotaka wewe, labda yeye naye hiyo ndiyo style yake.

Mbona Profesa Jay anaflow hivyo hivyo siku nyingi na watu wamemkubali kuwa hiyo ndiyo style yake?
Ndio style yake anayoweza hatukatai. Ila ili uwe competetive lazma uwe unawapa watu kitu kipya wasikuzoe style yako.
Ndo maana professor jay kwa hio style yake aliamua kupita kwenye Beat ya singeli ya shollo mwamba ilikua kama suprise maana hatukutegemea kutokana na alivyokua anaimba. Akipita tena kwenye amaPiano atatisha zaidi Respect kwake.

Unaona mfano Kala jeremiah yeye style ya kuimba na rap yake ileile watu wana mchoka na kum kinai masikioni mwao maana anachobadilisha ni message ila way ya ku flow na style ni ileile tangu atoke. Hvyohvyo ndo ikatokea kelele kwa young killer abadili flow maana game limebadilika
 
Sikiliza Ngoma zake angalau tatu uone kama magoti hayajakulegea
 
Pia mistari yake ni ya kichoko anajaribu kufurahisha lakini wapi, nadhani anamwiga maamuma mwenzake kontawa.
 
Kumwezesha ninakomaanisha siyo kusapotiwa bali kufundushwa jinsi ya kurap. Masela wa kitaa na mashabiki mandazi wanaweza kumsapoti mtu hata kama hajui kurap. Mbona Steve mweusi aliimba pumba liking alisapotiwa.
Mbona ka flow poa tu hapo kwenye Sir God.

Mtu akiwa hajarap unavyotaka wewe maana yake si kwamba hajui ku rap.

Ukisema hajui ku rap sema hajui kivipi, sema huyu hakai kwenye beat, hana vina, hana mizani, hana ujumbe.

Nimesikiliza wimbo wake mmoja "Sir God" nikakuta tofauti na nilivyotegemea kutokana na unavyomponda.

Amekaa kwenye beat vizuri, ana vina, anafuata mizani, kuna message nzuri tu uplifting alikuwa anaitoa.

Kama hajarap ulivyotaka wewe hiyo haimaanishi hajui ku rap, hiyo inqmaanisha hajatap unavyotaka wewe.

Wengine tulioanzisha hizo habari za ku rap Kiswahili tangu enzi za Hakim Mgomelo na Yo Rap Bonanza, wakati Too Proud anakuja mjini, wakati Nigga One anasoma International School of Tanganyika, wakati Sossy B anasumbua na Kukuru Kakara, wakati hata Profesa Jay hajaanza ku rap Hard Blasterz, wakati Kwanza Unit wanapanda Coco Beach, wakatiGWM wanarekodi "Cheza Mbali na Kashehe" kwa Bonny Love, tumeelewa anarap, anakwenda na beat, anaghani kwa vina na mizani, ana ujumbe.

Ikiwa hajarap unavyotaka wewe, hilo si sawa na kusema hajui ku rap.
 
Bila kupepesa macho kuna marapper na MCs msichanganye mambo na ndani ya Marappers pia kuana Marapper fake.
Naanza.
Real MCS
Tamaduni Music wote na Wasanii aina ya Fid Q na Wakongwe wengine na watu serious wanaojitambua.

Rappers
Wakali wanaomix miondoka mbalimbali Wasanii aina ya Stamina na Darasa, Billnass, Young killer nk Hawa nao sometimes miyayusho kama upo serious kama mimi maana wanacheza na upepo wa pesa.

Fake Rappers
Makatuni, Kizazi cha watoto mchelemchele Wasanii aina ya Bando, Kontawa, Lunya nk wanajikuta wapo serious wakati wanaimba upumbavu na hawana walijualo.

Nikishaona tu MwanahipHop anaandika matusi, anaimba vituko na hana Content za kujenga kichwa yangu mimi naachana nae siku hiyo hiyo.
 

Mi ni Shabiki sana wa Bando Na napenda style anayoimba Ni style Ya mziki ambayo ilianzishwa na Kina Juma nature na Kina KR huko Akaja akaiboresha Stamina..

Yaani kucheza na Maneno ila Mara Nyingine Rap katuni huwa Haina Ujumbe..

Ipa kwenye Hiyo nyimbo ya Sir God Naomba niende kinyime na wewe Kiranga kuwa Hiyo nyimbo kacopy Idea..

Ya Dax nyimbo inaitwa Dear God..


View: https://youtu.be/-Xe-b2zvPKE?si=roBTEWGNl5KNCzFX
 
Sikiliza Ngoma zake angalau tatu uone kama magoti hayajakulegea
S9hitaj8 kusikikiza ngoma tatu kujua kwamba lawama zako hazina msingi.

Ngoma moja tu inatisha kujua kwamba hata kama Bando si "King of Dar", ni kweli pia kuwa si mbaya kama unavyosema.

Ulivyomponda nilitegemea nisikie vichekesho vya mtu ambaye hata hawezi kwenda na beat.

Nikasikiliza "Sir God" na kujuta it's not that bad, ana style usiyoipenda tu.
 
Kumbe wewe promoter mkubwa
 
Ana viji maneno ambayo ukiviunganisha huwezi kuelewa anazungumzia nini. Jaribu kusikiliza Ngoma zake zingine uone mwenyewe
 
Mleta mada naomba unitajie Rapper wako bora.
Na vigezo unavyotumia ku Rate rap game?
 

Kwenye ku copy idea.

Guru wa Gangstarr katika "Take It Personal" ali rap hivi.

"Rap is an art, you can't own no loops
It's how you hook 'em up and the rhyme style, troop
So don't even think you could say someone bit
Off your weak beat, come on, you need to quit"
 
Mkuu ukisikia jinsia watu wnavyomsifia halafu ukaja kusikiliza Ngoma zake hata wewe ungemkinai maana sifa anazopewa na uhalisia wake ni vitu viwili tofati.
 
Ana viji maneno ambayo ukiviunganisha huwezi kuelewa anazungumzia nini. Jaribu kusikiliza Ngoma zake zingine uone mwenyewe
Sasa kama hujaelewa unajuaje yeye kakosea na sio wewe ndiye umekosea kuelewa?

Mimi nimesikiliza "Sir God" nikategemea kuvisikia vijimaneno hivyo, sikuvisikia.

Pia, si lazima umuelewe wewe, kama kuna watu wanamuelewa hiyo ndiyo crowd yake.

Na wewe tengeneza muziki wako kwa style yako upate washabiki wako.
 
Mkuu ukisikia jinsia watu wnavyomsifia halafu ukaja kusikiliza Ngoma zake hata wewe ungemkinai maana sifa anazopewa na uhalisia wake ni vitu viwili tofati.
Inaonekana kuwa watu wakimsifia wewe unaumia.

Kwa nini unaumia watu wakifurahia kitu wanachotaka kufurahia wao?

Toa nyimbo zako na wewe wanaopenda watakusifia tu.

Zako ziko wapi?
 
Inaonekana kuwa watu wakimsifia wewe unaumia.

Kwa nini unaumia watu wakifurahia kitu wanachotaka kufurahia wao?

Toa nyimbo zako na wewe wanaopenda watakusifia tu.

Zako ziko wapi?
Anaweza kuwa ndio Bando MC mwenyewe. Mambo kama ya freestyle ya Eminem kwenye 8 Mile movie, kujiponda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…