Sio Bongo yetu tu, hata huko Marekani kwa wenye Hip Hop yao sasa hivi imeingiliwa na vijana wa hivyo. Sasa hivi auto tune mwanzo mwisho na matusi kibao lakini wanachoongea akina sense yoyote.
Wakongwe kama 2PAC hata asipoimba, ukimpa microphone atoe speech unaweza ukatumia muda kumsikiliza.
Hata hata hapa kwetu wasanii waliosimama kidete mpaka wakabadilisha mtazamo wa wazee wetu kipindi hicho kwamba huu sio muziki wa kiuni nI watu ambao wamehudhuria vidato. Na maanisha watu kama Sugu, Solo Thang, Myalu, Mwana FA na wengineo.
Kwa mtazamo wangu, kwenye aina hii ya muziki, huwezi kuwa na ujumbe wa kueleweka kama hujawahi kusoma kitabu hata siku moja.