Msanii Barnaba atanisamehe katika hili

Msanii Barnaba atanisamehe katika hili

BIG Africa

Member
Joined
Oct 15, 2022
Posts
85
Reaction score
118
Habari zenu.Kwanza nianze kwa kusema kuwa simchukii msanii wa Bongo Fleva "Barnaba Boy". Nitakachokiandika hapa kinatokana na hisia zangu binafsi.

Ni hivi mimi Kwa uwezo wangu mdogo kuhusu mziki wa hapa nchini huwa namuona msanii Barnaba kama msanii mwenye juhudi zaidi lakini ana uwezo wa kawaida.

Ni msanii ambaye nyimbo zake nyingi ni za kawaida sana.Ninavyojua ni kwamba kuna wasanii vijana wadogo ambao wameanza mziki miaka michache iliyopita lakini wamekuwa wakitoa nyimbo Kali kuliko za Barnaba ambaye anaonekana ni mkongwe katika gemu ya mziki.Hawa ndio wakina Hamonize,Marioo na wengineo.

Narudia tena Barnaba huenda akawa ni msanii mkongwe nchi hii lakini anabakia kuwa msanii mwenye uwezo wa Kati au uwezo mdogo. Hii ni Kwa mujibu wa mtazamo wangu.

1689525260471.png

 
Mbona linajulikana ila hana nyota umekosea kumuongezea hilo.
 
Imagine nyimbo pekee ninayo iona kali ya huyu mwamba ni LOVER BOY tu. Nyingine zote naona kama za zuchu [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi binafsi toka niufahamu mziki huyo dogo ni mwanamziki ambaye sijawahi mkubali na wala sijawahi ona kama ni msanii mwenye uwezo mkubwa..alibebwa tu na Ruge.
 
Kuna wasanii na wanamuziki, mtu yeyote anaweza kuwa msanii ila ni ngumu sana kuwa mwanamziki.

Barnaba, Damian Soul Na Grace Matata ni miongoni mwa wanamziki wachache tulionao katika nchi hii.

Ukiupenda mziki, utampenda Barnaba.

Lover boy, I'm sorry, Isweke, Tunafanana na washa ni miongoni mwa vibao hatari sana kutoka kwa huyo Mwamba.

Ila huwa sivutiwi na lifestyle yake.
 
Back
Top Bottom