Msanii Belle 9 amewakosea nini Watanzania? Kwanini anapuuzwa? Ni wapi anakosea?

Msanii Belle 9 amewakosea nini Watanzania? Kwanini anapuuzwa? Ni wapi anakosea?

Muziki ni biashara huria sasa kua na bidhaa bora hakukupi guarantee Ya kufanya vizur moja kwa moja.
Lazma ufanye jitahda na maarifa ya kushawish wateja ubora wake ili pale watapoipata inakua rahs kuikubali na kukupa faida wewe.
Belle 9 kafeli hapa... anatoa mzki mzur lakn anakosa nguvu ya ushawish juu ya mzk wake..HITIMISHO:USIMAMIZI MBOVU
 
Hapa naona ni management!
 
Atafute ka skendo, hii tuu ndio dawa ya watz, mfano saa hivi Gwaijima atoe single itahit kinyama hata iwe mbovu kiasi gani.

Teh Teh Ngwajima atoe single...
 
Nakubaliana asilimia zote na wewe mkuu lakn kama msanii pia lazma ajue anachokiitaji.Management na yeye wamefeli pamoja.

Muda mwingine nafikiria kama amejitenga sana..na hafanyi juhudi binafsi kujipromote..
 
Jamaa namkubali sana.. Tena zaidi ya sana Lakini nilichogundua mziki wa bongo ili ufanye vizuri zaidi lazima uwe na sapoti nzuri mkoa unaotoka kitu ambacho Belle 9 hana..

Wasanii wengi wanaofanya vizuri bongo wakirudi home kwao ni wafalme.
 
Muda mwingine nafikiria kama amejitenga sana..na hafanyi juhudi binafsi kujipromote..

Ilo ndo tatizo siku hakilitatua hilo jamaa atakuja kua brand kubwa. Belle 9! Ni msanii ana jina kubwa lakn sio brand..Ney wa mitego ni msanii wa kawaida lkn sa hv ni brand sasa..unaweza ona ajabu lakn ndo dunia tuliopo sasa.
 
Huyu si ndio kamtoa Masogange ? basi ana nyota ya Punda ya kung'arisha wengine.

Ila labda kazi zake zinakuwa nyepesi sana...au hajishughulishi vya kutosha baada ya kutoa kazi...akishatoa ngoma anajifungia ndani na kubaki anasubiria zali.
 
Mkuu katika hili ntakupinga kidogo..mimi sifikiri kama clouds wanapaswa kupewa lawama au media yeyote kwa kuwa wao wanawapa walaji wanacho kitaka!

Kwa hiyo unataka kusema Clouds hawapigi nyimbo yake? Clouds wataipaje nyimbo air time ambayo haichaguliwi na walaji? Mbona kuna radio nyingi bongo na hata huko air time hazipewi vyakutosha?

Mkuu kuna ukweli katika hili kataa ukubali
Mziki wa Tz unashikiliwa na watu walijijengea mtandao fulani yaani bila wao utaishi patupu

Clouds ni wamojawapo wa hao madon wa Muziki tz

Belle9 alipoteza vibaya tu alipogombana na Cloud, kumbuka clouds inashirikiana na wanamtandao wanaoshirikiana kuendesha muziki wa bongo kwa maslahi yao

Sio belle9 tu, Juma nature yupo wapi? Unadhani akina temba ni wakali kuliko akina Juma neture?

Muziki wa bongo unafitna kubwa sana kuliko unavyodhaniwa wote wanaopotea wakati ni wakali wengi wao ni wale wanaopingana na mfumo huu gandamizi

Mfano Ay, Fa dimpoz chibu na wasanii wote wakali nk wakitoa ngoma lazima wawalipe fela na babutale eti ndio wasambazaji wa kazi kwenye media, jifanye kichwa ngumu sasa na upeleke mwenyewe uone kama zitapigwa hata mashabiki waombe marangapi,,,,,,, hazitapewa airtime ya kutosha

Prof Jay alitoa ngoma kali sana mbili kwa mpigo mwaka jana na tena alimshirikisha Chibu lakini kwasababu tu alikua upande wa Jide matokeo sote tunayajua

Mtu kama Tid mnyama na ujanja wake wote aliwaletea Clouds ujinga wakambania miezi kadhaa tu alirudi mbio kuwaomba msamaha na kwa jeuri wakamwambia ulitutukana habari maelezo rudi huko huko ukaonbee msamaha huko, na alirudi kweli

Tatizo hapa ni media zingine kushindwa kutumia fursa na kuwaacha clouds kumiliki wadau wote wa muziki kuanzia wadhamini hadi maboss wanaotoa shows na matangazo

Sasa kama nyimbo yako kali lakini haipigwi vyakutosha na haupati shows wala matangazo unategemea nini
Sikuhizi media zinalazimisha hata kama wimbo wa kawaida uonekane mzuri, utatangazwa utadhani nini na muhusika atapata shows na endorsements za kutosha iwapo tu atakubaliana na washika dau

Mimi naona ni makosa kudhani sisi watz ndio tunawaangusha wasanii bali ni mfumo fulani ambao wasanii wenyewe wanatakiwa wajitoe muhanga kupambambanao na sio sisi wlaji maana hatuna redio station wala hatundai shows
 
Huyu si ndio kamtoa Masogange ? basi ana nyota ya Punda ya kung'arisha wengine.

Ila labda kazi zake zinakuwa nyepesi sana...au hajishughulishi vya kutosha baada ya kutoa kazi...akishatoa ngoma anajifungia ndani na kubaki anasubiria zali.

Pengine kuna sehemu ana kosea lakini mimi nafikiri tatizo zaidi liko kwa management yake...
 
Mkuu kuna ukweli katika hili kataa ukubali
Mziki wa Tz unashikiliwa na watu walijijengea mtandao fulani yaani bila wao utaishi patupu

Clouds ni wamojawapo wa hao madon wa Muziki tz

Belle9 alipoteza vibaya tu alipogombana na Cloud, kumbuka clouds inashirikiana na wanamtandao wanaoshirikiana kuendesha muziki wa bongo kwa maslahi yao

Sio belle9 tu, Juma nature yupo wapi? Unadhani akina temba ni wakali kuliko akina Juma neture?

Muziki wa bongo unafitna kubwa sana kuliko unavyodhaniwa wote wanaopotea wakati ni wakali wengi wao ni wale wanaopingana na mfumo huu gandamizi

Mfano Ay, Fa dimpoz chibu na wasanii wote wakali nk wakitoa ngoma lazima wawalipe fela na babutale eti ndio wasambazaji wa kazi kwenye media, jifanye kichwa ngumu sasa na upeleke mwenyewe uone kama zitapigwa hata mashabiki waombe marangapi,,,,,,, hazitapewa airtime ya kutosha

Prof Jay alitoa ngoma kali sana mbili kwa mpigo mwaka jana na tena alimshirikisha Chibu lakini kwasababu tu alikua upande wa Jide matokeo sote tunayajua

Mtu kama Tid mnyama na ujanja wake wote aliwaletea Clouds ujinga wakambania miezi kadhaa tu alirudi mbio kuwaomba msamaha na kwa jeuri wakamwambia ulitutukana habari maelezo rudi huko huko ukaonbee msamaha huko, na alirudi kweli

Tatizo hapa ni media zingine kushindwa kutumia fursa na kuwaacha clouds kumiliki wadau wote wa muziki kuanzia wadhamini hadi maboss wanaotoa shows na matangazo

Sasa kama nyimbo yako kali lakini haipigwi vyakutosha na haupati shows wala matangazo unategemea nini
Sikuhizi media zinalazimisha hata kama wimbo wa kawaida uonekane mzuri, utatangazwa utadhani nini na muhusika atapata shows na endorsements za kutosha iwapo tu atakubaliana na washika dau

Mimi naona ni makosa kudhani sisi watz ndio tunawaangusha wasanii bali ni mfumo fulani ambao wasanii wenyewe wanatakiwa wajitoe muhanga kupambambanao na sio sisi wlaji maana hatuna redio station wala hatundai shows

Mbona sioni kama Bell 9 ana tatizo na Clouds? Mbona nyimbo yake.hupigwa?
 
Belle aliwahi kuhit sana kipindi ndo anatoka, song zake 2 'Sumu ya penzi' na 'Masogange' zilihit na kumpatia shows za kutosha. Kimavi kilianza baada ya ujio wa Diamond, alipoanza kupambanishwa na Diamond mi nahisi ndo ilikuwa gundu kwake kozi Diamond kila kukicha alikuwa anazid kung'ara huku Belle taratiibu akianza kupotezewa, yaani ni kama Diamond alikuja na nyota yake then akaongeza nyingine kwa kuipora ya Belle. Mi naamini kabisa asingekuwepo Diamond kwenye game Belle angekuwa mbali sana, Diamond ndo kamletea kimavi, Belle anajua sana hilo halina ubishi ila ndo hivo tena
 
Wana jamvi wasalaam...
Wana jamvi katika adhabu ambayo anaweza kupewa mtu na ikamuumiza sana na akashindwa kujua la kufanya au suluhu ni adhabu ya kupuuzwa.

Adhabu ya kupuuzwa ndio aliyo pewa msanii Bell 9 na watanzania walio wadau wa muziki!
Bell 9 ni mmoja wa wasanii wenye sauti nzuri,mtunzi mzuri na mwimbaji mzuri lakini hakuwai kufurahia matunda ya kipaji chake kama wengine!

Bell 9 pamoja nakujua hayo yote na baadhi ya watanzania kusifu nyimbo zake lakini zimekuwa zikikosa muda wa hewani wa kutosha kama nyimbo nyingine na ni vigumu nyimbo kupata muda wa hewani kwenye radio station na Tv kama walaji hawauchagui wimbo husika!
Watanzania, Bell 9 amewakosea nini? Kwanini mna mpuuza kiasi hiki? Pamoja na msanii huyu kutoa wimbo mpya hivi karibuni lakini kwa utafiti nilio ufanya mapokeo yake ni madogo na ya kukatisha tamaa pamoja na wimbo husika kuwa mzuri sana.

Msanii Bell 9 anakosea wapi?
Aina ya studio anayo record?
Aina ya management aliyo nayo?
Aina ya utunzi anao utumia au nyimbo anazo imba?
Amejiweka mbali na mashabiki?
Kwakuwa hana kick au scandal?

Nimejiuliza maswali mengi lakini nimekosa majibu kabisa juu ya msanii huyu Bell 9 na huwa namuonea huruma pamoja na kuonesha juhudi lakini ana puuzwa sana ....hakika kwa jinsi anavyo puuzwa huyu msanii ningekuwa ndugu yake ninge mshauri atafute shughuli nyingine ya kufanya.
Kuna nyimbo zinapata air time ya kutosha hadi una shangaa huyu Bell 9 ana shida gani?

Msanii Bell 9 amewakosea nini watanzania? ni wapi ana kosea?
Karibuni wana jamvi.

Mkuu kuna mtasha mmoja tupo nae uku mtwara alikuwa anaisikilizia nyimbo ya listen ya bele 9, hakujua km ni msanii wa tz, nilivyomjulisha alistaajabu sana akasema ile nyimbo ni level za juu sana! BTW niseme tatzo kuna miungu watu wameshikilia soko la muziki usipowaabudia ndio hivyo ila binafsi katka wasanii watatu tz belle 9 yumo anajua sana!
 
Unataka atoke vipi mkuu,,,, ?? mbona yuko vizuri tu. Sema hajipendekezi kwa kina Ruge kama wafanyavyo wa kina Neema. anaijua thamani yake na sisi tunaejua uwezo wake tuko poa nae.
 
Back
Top Bottom