BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mwanamuziki, Lameck Ditto amewasilisha vielelezo tisa wakati akitoa ushahidi katika kesi ya madai dhidi kampuni ya Multichoice Tanzania Limited, akiituhumu kutumia wimbo wake bila ridhaa yake katika kipindi cha kampeni ya Afcon 2019.
Ditto ambaye jina lake halisi ni Dotto Bernard Bwakeya ameiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iamuru kampuni hiyo imlipe fidia ya Sh6 bilioni kwa kutumia wimbo wa 'Nchi Yangu' aliodai ni wake kwenye matangazo yao ya biashara bila ridhaa yake.
Pia ameiomba Mahakama iamuru alipwe Sh200 milioni kutokana na madhara ya jumla, lakini pia alipwe riba ya asilimia 25 tangu siku alipofungua shauri hilo.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya shauri hilo, Wakili wa Ditto, Elizabeth Mlemeta amesema kesi hiyo imeanza kusikilizwa na upande wa mdai una mashahidi watano.
Pia, Soma=> Lameck Ditto achemka madai ya bilioni 6 dhidi ya DStv, Mahakama yasema ilitumika 'second version' na si 'original' yake