Msanii Ditto afungua kesi ya Madai ya Tsh. Bilioni 6 dhidi ya Multi Choice (DSTV)

Msanii Ditto afungua kesi ya Madai ya Tsh. Bilioni 6 dhidi ya Multi Choice (DSTV)

Na unaweza shangaa akalipwa.

Hizi dili wasanii huwa wanafanya na wafanyakazi wa hizo kampuni wanazozidai.

Hela za kampuni kila mtu anazitaka. Hata wafanyakazi wa hizo kampuni wanazitaka hizo bilioni za mwajiri wao
Swali la msingi ni je anachodai kina merit? Hayo mengine ni speculation tu. Kama DSTV wali-violate rights za Ditto lazima washikwe koo, regardless how.
 
View attachment 2822700
Mwanamuziki, Lameck Ditto amewasilisha vielelezo tisa wakati akitoa ushahidi katika kesi ya madai dhidi kampuni ya Multichoice Tanzania Limited, akiituhumu kutumia wimbo wake bila ridhaa yake katika kipindi cha kampeni ya Afcon 2019.

Ditto ambaye jina lake halisi ni Dotto Bernard Bwakeya ameiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iamuru kampuni hiyo imlipe fidia ya Sh6 bilioni kwa kutumia wimbo wa 'Nchi Yangu' aliodai ni wake kwenye matangazo yao ya biashara bila ridhaa yake.

Pia ameiomba Mahakama iamuru alipwe Sh200 milioni kutokana na madhara ya jumla, lakini pia alipwe riba ya asilimia 25 tangu siku alipofungua shauri hilo.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya shauri hilo, Wakili wa Ditto, Elizabeth Mlemeta amesema kesi hiyo imeanza kusikilizwa na upande wa mdai una mashahidi watano.
🤣🤣
 
Wabongo bwana nyimbo zenu zisipopigwa mnapiga kelele mnabaniwa. Zikipigwa ndio mnajitutumua. Mbona zinapigwa kwenye bar za pombe za kienyeji hamdai fidia?
Hakuna tatizo ni kwa ruhusa yanani mf. Mkeo umkute anampikia jirani nakumlisha halafu jirani anakuambia kwani kuna ubaya gani??
Eti ubaya?? Ndio kuna ubaya kwa sababu ni kwa ruhusa ya nani
 
Inapopigwa kwenye baa inatangaza nini?

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Inatangaza biashara ya pombe ili walevi wajaze na mwenye bar 🍺 aingize kipato atajirike wakati aliyeutunga anadhindia mihogo na hata akienda kwenye hiyo bar hawezi kupewa hata bia ya bure. Na hii ni kwa magari yote ya promotion
 
Na unaweza shangaa akalipwa.

Hizi dili wasanii huwa wanafanya na wafanyakazi wa hizo kampuni wanazozidai.

Hela za kampuni kila mtu anazitaka. Hata wafanyakazi wa hizo kampuni wanazitaka hizo bilioni za mwajiri wao
Sasa billion 6 kwa DStv kitu unajua wanaingiza Pesa kiasi gan?
 
Back
Top Bottom