Msanii gani maarufu umewahi kuonana naye live mkaongea mawili matatu

Enzi hizo nasoma english course kwa ras Simba magomeni mapipa pale nikakutana na Dogo Janja na yeye sijui alikuwa anataka kusoma pale? Na joti niliwahi muona Happ.
Mirror nimepiga nae Sana story tulikuwa tunakaa Mtaa mmoja maeneo ya Buguruni enzi hizo hajatoa hata ngoma Moja.
Q chief aliwahi pita na kibajaji maeneo ya kinondoni pale nikamuuzia sigara!
(Nilikuwa nauza kiduka flani hapo)
Barnaba nishamuona mara nyingi tu pale White Rose sema hatukuwahi kuongea chochote.
Dr cheni, Aika wa Navy kenzo, Nyoshi el Sadaat, Abdu kiba, Shamsa Ford, Chidi Mapenzi, Patcho Mwamba, ,Jimmy Mafufu, Mr Blue Mitaa ya tabata kimanga kule, Dully sykes etc.
 
Yvonne Paul mshindi wa tano nadhani tulikuwa classmates O level.
Alikuwaga head girl shuleni.
 
Mkuu unasubiri picha ya pamoja? Tia vokali
 
unakaa buguruni ipi?
 
2018 nimekutana ba Belle 9 naelekea mwanza nimepanda kisbo tulikaa sit moja yeye alipandia moro akashuka dodoma.muongeaji kawaida tu ila alikua anajishtukia shtukia sasa sijui why...ila usanii ni kazi ngumu sanaa
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Mwezi Desemba 2017, natoka Cairo nilikuwa naunganisha ndege Addis Ababa kurudi DSM, nilikutana na Asley akaniamkia Shikamoo nami nikamuitikia Marahaba. Hayo ni maneno mawili tayari, neno la tatu halikuwepo.
 
Dully sykes zamani sana alikuwa mshikaji nadhani ilikuwa around 2002 au 2003 wakati huo anatembea na "ATU" ,cha kusikitisha ATU alifariki kwa "NGOMA".

Father Nelly alikuwa msela wangu sana enzi hizo wakati nakaa "NGALIMI".

Mkuu kumbe una age pengine ni moja ya ma Bro ninaowajua. RIP, Faza Nelly.
 
Songa
Sio kuongea nae tu huyu nimesoma nae toka vidudu/nursery hadi darasa la 4.

Chege, Temba hawa walikuja miaka hiyo ya 2003 kushot video yao Kwenye kota za jeshi sasa wakadhani wataweza kufanya jambo lao kirahisi,
wakakataliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…