TANZIA Msanii Golden Jacob Mbunda(Godzilla) afariki dunia

Nilitamani siku moja nije nisikie jinsi game inavyochange remix labda ungeweza kuonesha hisia zako halisi!!
Najua huwezi kuona ila hata wale waliokuwa wanapambana kukuangusha kimuziki/kimaisha nao wamefika salasala kukuaga bro!!
 
Joyce Mbunda, dada wa mwanamuziki wa Hip Hop, Godzillah aliyefariki dunia leo Jumatano Februari 13, 2019 amesema ndugu yake aliteswa na kitu kilichokwama tumboni kwa zaidi ya siku tatu na kumfanya atapike mfululizo.

Akizungumza leo nyumbani kwao Salasala jijini Dar es Salaam, Joyce amesema mwanamuziki huyo Golden Mbunda alikuwa akitapika kwa siku tatu mfululizo.

Amesema rapa huyo aliyewahi kutamba na wimbo Lakuchumpa alianza kujisikia vibaya na alipokwenda hospitali alibainika kuwa na malaria, sukari kuwa juu na presha.

Jumapili (Februari 10, 2019) alilala muda mrefu, haikuwa kawaida. Baadaye akaomba barafu tulivyompa akaanza kutapika ndipo tulipompeleka hospitali na kugundulika ana malaria, sukari imepanda sana na presha imeshuka,” amesema.

Pia marehemu alisema kuna kitu kiling’ang’ania tumboni kama vile kinataka kutoka ila kinagoma, alijaribu kukitoa kwa kujitapisha lakini hakikutoka.”

Pamoja na kupata nafuu baada ya matibabu alilalamika kitu hicho kuendelea kukwama tumboni.

Alipewa ruhusa ingawa alikuwa anaendelea kutapika. Usiku akaanza kuishiwa nguvu. Tukamrudisha hospitali akawekewa dripu mwisho akaandikiwa dozi ya siku 10. Alipofika nyumbani alisali kabla ya kuingia kulala lakini haikuchukua dakika 10 akaanza kuniita,” amesema.

Nilimfuata chumbani nikiwa na mama, akatuambia naona watu wengi wananifuata wamezunguka nyumba wanataka kunichukua. Akainuka ghafla akasema acha nitoke nje, tukamshika maana alikuwa anaihangaika akamlalia mama na hakuinuka tena.”

Amesema walimpeleka hospitali ya jeshi ya Lugalo wakiamini kuwa anaweza kuwa amezimia tu lakini waliambiwa amefariki dunia.

Source:Mwanaspoti
 
Nmehuzunika , nimelia !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyongo hiyo, na hizi pombe za vjana
 
Malaria na dawa zake zinatabia ya kutibua ini...kabla ya kupona lazima utapike sana nyongo...yashianikuta...kwa wale wanaopataga malaria mara moja moja baada ya miaka mingi watanielewa...inaibukaga ghafla yani si mchezo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amefia miguun kwa mama ake masikin ndio maana video zinaonesha mama ake analia kwa uchungu sana haamin mwanae kumtoka[emoji22][emoji22]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alitumia beat ya wimbo wa "Otis" Kanye & Jay Z

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Za asubuh wana Jf ikiwa imepita siku moja taarifa za aliekuwa msanii bora wa free style lakini nyuma kabla ya hapo ilifika kipindi ikawa kama Kapagawa. Kisa penzi la mwanadada fulani kwa mtazamo wangu na hili Lili kuwa chanzo cha pressure iliopelekea taarifa hizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…