Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Vitu vingine ushamba tuuInadaiwa Msanii Harmonize na team yake ya Konde Gang walienda VVIP kwa ajili ya kushuhudia mchezo wa Tanzania dhidi ya Morocco kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026, wakati wa mapumziko, jana Usiku wa Novemba 21, 2023.
Watu hao wakashuka kwa lengo la kuelekea Uwanjani inaaminika wlaitaka kwenda kutoa hamasa kwa mashabiki wa Tanzania kuendelea kuishangilia timu yao lakini walinzi (Mabaunsa) waliwakatalia.
Wakati ubishani ukiendelea, ghafla kuna Baunsa akampiga ngumi Harmonize ambaye naye akarudisha na kuzuka kwa vurugu kwa dakika kadhaa.
Baada ya vuta nikuvute ya zaidi ya dkika 10 ndipo Askari Polisi wakafika na kumaliza mzozo huo.
Sent using Jamii Forums mobile app