Msanii Ibra wa Mmakonde karudi nyuma hatua 70

Madimba jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2017
Posts
1,577
Reaction score
3,146
Huyu bwa mdogo alianza vyema lakini sasa hivi anazidi kudrop, wimbo wake mpya haueleweki, haufanyi vizuri sokoni, promo kutoka kwa boss wake hapati ya kutosha..kaporomoka hatua 70 nyuma, ni vyema ajitafakari uwepo wake pale KM una tija yoyote?
 
Harmonize ana kurupuka yeye mwenyewe mwaka huu katoa album yenye nyimbo 18 zote zinatakiwa kupushiwa lkn cha ajabu naona album kaachana nayo mwezi uliopita katoa single jeshi,na mwezi huu katangaza anaachia nyimbo nyingine,sasa huyo Ibra atasikilizwa saa ngapi wakati anashindwa kumpa nafasi baada ampush dogo anapushi nyimbo zake.

Haya Ibra tia maji tia maji,unakuja kutangaza wasanii wapya watatu Cheed,Country boy na Killy hawa wote wana hitaji promo yaani anazidi kuivuruga biashara yake ,anashindwa kutengeneza plan kwa ajili ya kuwasimamisha wasanii wake.

Mwisho wa siku hii label kwa mwendo huu itakuja kusababisha ugomvi mkubwa sana kati ya Harmonize na Jembe ni Jembe sababu wataweka hela nyingi ambayo hazitakuja kurudi sababu tu ya mipango yao mibovu kwa wasanii wao.
 
Hayo ni makasiriko sasa
Kisa tu wimbo hujauelewa wewe unajumuisha wote hawauelewi.?

Labda kwenye promo wamezingua sawa
Ila ibrah anajua sanaaa
Kakosa tu promo nzuri
 
Hayo ni makasiriko sasa
Kisa tu wimbo hujauelewa wewe unajumuisha wote hawauelewi.?

Labda kwenye promo wamezingua sawa
Ila ibrah anajua sanaaa
Kakosa tu promo nzuri
Ibra atapewa vipi promo wakati bosi wake kila siku anaachia nyimbo,kila mwezi anatambulisha msanii mpya,huyo Ibra atasikilizwa saa ngapi.

Wanachemka wenyewe kwenye mipango yao.
 
Ibra atapewa vipi promo wakati bosi wake kila siku anaachia nyimbo,kila mwezi anatambulisha msanii mpya,huyo Ibra atasikilizwa saa ngapi.

Wanachemka wenyewe kwenye mipango yao.
Ndo maana nimesema ibrah anahitaji promo.tu ni msaniii mkali
Ila nawe umezidisha chumvi eti kila mwezi msanii mpya ..
Hahahhaah
Anzia kuhesabu toka mwezi wa kwanza mpka sasa si wangekuwa 10
Hahahah
 
Ndo maana nimesema ibrah anahitaji promo.tu ni msaniii mkali
Ila nawe umezidisha chumvi eti kila mwezi msanii mpya ..
Hahahhaah
Anzia kuhesabu toka mwezi wa kwanza mpka sasa si wangekuwa 10
Hahahah
Kwa wasanii wapya waliotoka huyo dogo mpaka sasa ndio the best.

Kama ni tuzo kwa upcoming artist huyo dogo anastahili.

Sijachelewa ni bonge la ngoma kuanzia mashairi, utunzi na mdundo.

Ni purely bongo fleva.
 
Halafu kuna jamaa hapa anasema eti nyimbo haieleweki
Hii ngoma imesikilizwa sana tu ubaya wetu wabongo tunaenda kwa DJ mwanga kudownload bure so takwimu halisi hazionekani
 
Halafu kuna jamaa hapa anasema eti nyimbo haieleweki
Hii ngoma imesikilizwa sana tu ubaya wetu wabongo tunaenda kwa DJ mwanga kudownload bure so takwimu halisi hazionekani
Kuna watu ni mashabiki lialia, hawawezi kujua muziki.

Mtu tangu asubuhi mpaka jioni kaweka Wasafi TV/FM instagram anawafollow Wasafi tu hawezi kujua muziki nje ya circle hiyo.

Huyo dogo hata akiachwa hapo Konde music hatakosa msimamizi.

Uwezo wake ushaonekana
 
Huyu jamaa anajua sana ila management aliyonayo haina kichwa!! Yani kondegang ni kikundi tu cha wahun uendeshaji wake haupo focused!!
 
Hayo ni makasiriko sasa
Kisa tu wimbo hujauelewa wewe unajumuisha wote hawauelewi.?

Labda kwenye promo wamezingua sawa
Ila ibrah anajua sanaaa
Kakosa tu promo nzuri
Akipata promo nzuri mtasema anabebwa na promo which is which?
 
Ndo maana nimesema ibrah anahitaji promo.tu ni msaniii mkali
Ila nawe umezidisha chumvi eti kila mwezi msanii mpya ..
Hahahhaah
Anzia kuhesabu toka mwezi wa kwanza mpka sasa si wangekuwa 10
Hahahah
🤣🤣🤣 ila hawako organize kutoka mwezi wa 4 mpaka sasa washatambulisha wasanii wanne,yeye mwenyewe sasa kila siku ana achia nyimbo zake.Lazima wa kwame.Wana mipango mingi ambayo mwisho wa siku haitekelezeki.

Miezi miwili iliyo pita Harmonize na EFM (Bdozen na Majizo) walisema wataandaa show Uhuru kwa siku tatu mfululizo kuanzia tar 7 mpaka 10 November 2020,lkn ukitizama mpaka sasa hata dalili hamna.

Wale Cheed na Killy walitakiwa watoke mwishoni mwa mwaka kesho au kesho kutwa tena kwa awamu,yy wote kawatambulisha August na sijui watawa promoti vipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…