Harmonize ana kurupuka yeye mwenyewe mwaka huu katoa album yenye nyimbo 18 zote zinatakiwa kupushiwa lkn cha ajabu naona album kaachana nayo mwezi uliopita katoa single jeshi,na mwezi huu katangaza anaachia nyimbo nyingine,sasa huyo Ibra atasikilizwa saa ngapi wakati anashindwa kumpa nafasi baada ampush dogo anapushi nyimbo zake.
Haya Ibra tia maji tia maji,unakuja kutangaza wasanii wapya watatu Cheed,Country boy na Killy hawa wote wana hitaji promo yaani anazidi kuivuruga biashara yake ,anashindwa kutengeneza plan kwa ajili ya kuwasimamisha wasanii wake.
Mwisho wa siku hii label kwa mwendo huu itakuja kusababisha ugomvi mkubwa sana kati ya Harmonize na Jembe ni Jembe sababu wataweka hela nyingi ambayo hazitakuja kurudi sababu tu ya mipango yao mibovu kwa wasanii wao.