makedonia
JF-Expert Member
- Nov 17, 2014
- 4,371
- 3,670
Msanii wa maigizo Jimmy Mafufu amesema ushiriki wa wasanii katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu haukuwa kosa, akibainisha kuwa walitumia haki yao ya kikatiba, hivyo hawana sababu yoyote ya kuomba radhi kwa yeyote.
Kauli hiyo ya Mafufu imekuja wakati ambapo mjadala mkali unaendelea katika mitandao ya kijamii, baada ya madai ya kuzorota kwa mauzo ya kazi za wasanii baadhi ya wadau wakihusisha hali hiyo na msimamo wa baadhi ya wasanii katika kipindi cha kampeni.
Wadau mbalimbali wa sekta ya sanaa wameendelea kutoa maoni yao kuhusu changamoto hizo, akiwemo msanii Rajabu Ibrahim ‘Harmonize’ pamoja na Mkurugenzi wa EFM na TVE, Francis Ciza ‘Majizo’, ambao wote wametoa mitazamo tofauti kuhusu mustakabali wa biashara ya sanaa nchini.
Mafufu amesisitiza kuwa badala ya kulaumiana, sekta ya sanaa inapaswa kujikita katika mbinu mpya za kuongeza thamani ya kazi zao na kuboresha uhusiano na mashabiki
Ndio linani hilo mbona hatulijui !!!
PUMBAVU