Leo nikiwa napita mitaa ya Sinza kumekucha jirani na geti la Law aSchool of Tanzania nimekutana USO kwa USO na msanii Jocelyn akiwa anauza chips.Jocelyn alitamba sana miaka ya 2005 na 2006 na nyimbo zake Perfume na Niite Basi.
Pia aliwahi kushirikishwa kwenye wimbo wa Msanii Duly Sykes uitwao Dhahabu ambamo ndani yake alishirikishwa pia Mr.Blue..Big up sana kwa msanii Jocelyn kwa kuingia kwenye ujasiriamali.
Binafsi nimefurahishwa sana na hustling spirit yako...Pia hongera kwa kupata goli hapo LST kwa sababu ni sehemu ambayo kuna idadi kubwa sana ya wateja