Msanii Joslin anauza chipsi Sinza Kumekucha

Msanii Joslin anauza chipsi Sinza Kumekucha

Feruzi nae alionekana anatembeza dagaa bichi... kumbe ni ujio wa nyimbo yake mpya...

Sasa ni kwa Joslin siyo...

Ni kawaida sana kwa binadamu kujishughulisha...

Kuna msanii mmoja wa kike mrembo hivi na ni maarufu, anatembeza biashara kwenye maofisi...


Cc: mahondaw
 
Huyu Joslin ana wimbo wake mmoja unahusu ukimwi,huo wimbo unaelezea rafiki yake mmoja alipima ngoma akajikuta hana,akaandaa pati kufurahia afya yake,kwenye hiyo pati akakutana na mwanamke na kuondoka nae,kumbe yule mwanamke alikua ana ngoma! Mwenye kuujua huu wimbo aniwekee hapa kisha anitag,nitashukuru sana.
 
Mi nilisha wahi muona hapo nikajua namfananisha kumbe ndie... Sasa asiendekeze mademu pale watamfilisi maana wana njaa hao...
 
Bora jamaa anakomaa kiume kuliko PNC ,aliyekuwa analialia.Haya ndio maisha hayana formula,ila ndio utajua hapa bongo hamna washabiki bali oya oya ndio wapo kibao na wale washikadau walio mtumia wamemsusa sasa hivi anapambambana peke yake ndio maisha yalivyo.
@PNC 1
 
Mtoa mada ni mnafiki sana aisee. Hivi hujui kuwa hata Masanja anauza chakula, Jide aliuza chakula, Shilole anauza chakula. Leo Joslin anauza chakula unamkebehi si bure una roho mbaya sana
 
Hongera kwake na vijana wengine waige, si vyema kung'ang'ania fani ambayo haina tija kwa kuwa umepata umaarufu tu, hata vijana mnaomaliza vyuo vikuu kama hujaajiliwa kaanga tu mihogo ili mradi upate kipato. Ni aibu kupiga piga mizinga ikiwa shughuli za kufanya zipo
 
Back
Top Bottom