OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Msanii Mkongwe wa Bongo Fleva, Juma Kassim'Nature' ametoa misaada mbalimbali kwenye hospitali ya Zakhem iliyopo maeneo ya Mbagala jijini Dar.
Akizungumza na Clouds FM, alisema kuwa ameamua kutoa misaada hiyo kwa kuwa hospitali hiyo ipo katika eneo analoishi na yeye huwa anatibiwa hapo na kuona kuna mahitaji muhimu yanayohitajika kwenye hospitali hiyo.
Misaada aliyoitoa ni pamoja na vyakula, mashuka, sabuni na juisi mbalimbali na pia ametoa ushauri kwa wasanii mbalimbali kuikumbuka jamii kwa kutoa misaada.